JE? WAJUA MWENYEKITI WA CHADEMA KAGERA AMEWAHI KUKABILIWA NA KESI YA UHUJUMU UCHUMI?




Baada ya kuchaguliwa uenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kagera, bosi wa zamani wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mkoba amesema vipaumbele atakavyoanza navyo ni kuamsha ari ya wanachama wa chama hicho, kikokotoo, Katiba mpya, Tume huru, bima ya afya na elimu atakayoyatekeleza kwa ushirikiano na viongozi wenzake wa mkoa na Taifa wa Chadema.


Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema alimtangaza Mkoba kushinda nafasi hiyo, baada ya kupata kura za ndio 50 kati ya 55 za wajumbe waliohudhuria mkutano huo kwa siku ya Jumapili.


Ikumbukwe kuwa Mkoba aliyewahi kuwa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) nafasi aliyoikaimu kuanzia mwaka 2012-2017 na enzi za uenyekiti wake aliwahi kuwa na mgogororo katika kipindi cha Rais wa awamu tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa kesi ya ubadhirifu wa mali za umma.

Mkoba alikuwa mgombea pekee wa uenyekiti baada ya mshindani wake Justus Basheka kuenguliwa na kamati ya usahili kwa sababu mbalimbali.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA