KITENDO CHA PADRE KUJILAZA KIFUDIFUDI MBELE YA ALTARE

 



Mwanzoni mwa Ibada ya Mateso ya Bwana siku ya Ijumaa Kuu Padre hufika na kujilaza kifudifudi (anaweza pia kupiga magoti yote mawili).

Tendo hili lina maana kubwa tatu: kwanza, kuonesha anguko la wazazi wetu wa kwanza Adamu na Eva. Anguko hilo ndilo limesababisha sisi kuendelea kuanguka dhambini.

Pili, kujilaza kifudifudi ni ishara inayoonesha fedheha aliyoipata mwanadamu baada ya kuanguka dhambini na hivyo anaonesha unyonge wake mbele ya Mungu (the abasement of earthly man).

Tatu, kujilaza kifudifudi ni ishara inayoonesha pia huzuni na maumivu ya kanisa juu ya mateso yaliyompata Kristo.

Nyongeza: Wakati wa Ibada ya Upadrisho au Uaskofisho, Padre/Askofu mteule hujilaza kifudifudi mbele ya Altare. Tendo hili huonesha hali yake ya kutokustahili kupewa huduma husika (unworthiness in carrying the ministry) na hivyo anajiaminisha kwa Mungu na kuomba msaada wa maombezi ya watakatifu (ndiyo maana wakati huo huimbwa Litania ya Watakatifu) ili aweze kuhudumu vema katika huduma anayopewa.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA