Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amewasili wilayani Tarime, Mkoa wa Mara, kushiriki mazishi ya Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC), Jimbo la Mara Kaskazini, Bi. Francisca Mwita Gachuma, ambaye ni mwenza wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, Ndugu Christopher Mwita Gachuma.
Baada ya kuwasili msibani nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Bomani, Tarime Mjini, leo Ijumaa, Machi 29, 2024, na kupokelewa na Viongozi wa Chama na Serikali, Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi alipata fursa ya kuweka saini kitabu cha maombolezo na kuwapatia pole wafiwa, wakiongozwa na Familia ya Mzee Gachuma, pamoja na kushiriki ratiba ya awali ya msiba, kabla ya mazishi yatakayofanyika Machi 30, 2024, huko Komaswa, Tarime.
إرسال تعليق