Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka miradi mingi ya maendeleo katika Jimbo hilo Mkoani Kagera.
Kauli hiyo ni kufuatia Ziara ya zaidi ya Kata 20 ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ndaisaba George Ruhoro za Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera iliyokuwa na Dhima ya Kusikiliza na kutatua kero za wananchi hao katika sekta ya Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.
Pamoja na mambo mengine ameelezea baadhi ya miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika sekta ya Elimu, Afya, Maji, Miundombinu ya barabara n.k huku akiwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani pamoja na changamoto zilizopo zinatokana na hatua za maendeleo walizopiga tangu Mwaka 2020 na hivyo anaimani zitaisha na zitabakikuwa historia.
"Niwaombe wananchi wa Ngara endeleeni kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wenu kwani mengi tumeyafanya na Maendeleo ni hatua, na hatua moja huanzisha hatua nyingin, Rais wetu kipenzi cha watanzania amefikisha miaka mitatu tangu aingie madarakani. Wananchi wa Jimbo la Ngara wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Ngara, Ndaisaba George Ruhoro tumeazimia kumpa kura nyingi mwaka 2025, ametufanyia mambo makubwa sisi Wananchi wa Ngara" Amesema Mbunge huyo
Amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa Bilioni 100 kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Lami kutoka Nyakahora mpaka Rusumo katika jimbo la Ngara.
"Rais Samia ametoa Shilingi Bilioni 100 kwaajili ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka Nyakahora mpaka Rusumo katika Jimbo la Ngara, mradi huu umeanza kujengwa na Mkandarasi yupo Site. Ni Mama yetu, kipenzi cha Watanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan" Alisema Mbunge Ndaisaba
Katika sekta ya umeme, amewataka wananchi wa Mumilamila kuwa na subra kwani tayari Mkandarasi yuko 'Site' na hadi kufikia mwaka 2025 umeme utakuwa umewafikia.
"Rais Samia ametoa zaidi ya Shilingi Bilioni 11 katika kipindi cha miaka mitatu hapa Ngara kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya umeme. Umeme uko unakuja, Mkandarasi yuko site, nguzo zinaendelea kusogea, anatakiwa alete nyaya afunge transformer awashe umeme. Mpaka kufikia mwaka 2025 umeme utakuwa umewaka hapa Mumilamila" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
Katika sekta ya Maji amesema "Rais Samia katika kipindi cha miaka mitatu ametoa zaidi ya Shilingi Bilioni 8 kwaajili ya ujenzi wa miradi ya Maji mpaka mradi wa Maji wa Bugarama ni sehemu ya fedha alizotoa Rais. Mradi umejengwa, umekamilika na unatoa Maji" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
Sanjari na hayo katika sekta ya Afya na miundombinu ya barabara ameelezea utekelezaji wake ambapo mpaka sasa tayari Bilioni 2 zimeshatolewa kati ya Bilioni 3 kwaajili ya Hospitali ya Wilaya inayoendelea kujengwa Mbuba, Barabara ya kutoka Bugarama mpaka Kabanga Nickel (Km 7.9) imetengewa Shilingi Milioni 8.98. Barabara ya kutoka Lunyana - Kihinga - Nyarukubala - Nyarulama imetengewa Shilingi Milioni 27.28. Barabara ya Nyarulama Sokoni - Mukivumu - Mumilamila Centre imetengewa Shilingi Milioni 27.9 kwaajili ya matengenezo.
"Mama Samia nilimkimbilia, nikasema watu wa Bushubi, Bugarama, Kihinga na Mumilamila wanapoenda hospitali ya Wilaya wanateseka sana wengine wanafia njiani kwasababu ya umbali mrefu wa kusafiri zaidi ya Kilomita 70. Rais Samia amenipa Bilioni 2 kati ya Bilioni 3 alizoahidi kutoa na Hospitali ya Wilaya inaendelea kujengwa Mbuba" Alisema Mhe. Ndaisaba George Ruhoro
"Barabara ya kutoka Bugarama mpaka Kabanga Nickel (Km 7.9) imetengewa Shilingi Milioni 8.98. Barabara ya kutoka Lunyana - Kihinga - Nyarukubala - Nyarulama imetengewa Shilingi Milioni 27.28. Barabara ya Nyarulama Sokoni - Mukivumu - Mumilamila Centre imetengewa Shilingi Milioni 27.9 kwaajili ya matengenezo" Alisema Mbunge wa Jimbo la Ngara.
Hata hivyo Ziara ya Mbunge huyo iliyokuwa na dhima ya kuelezea utekelezaji wa mirada ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za wananchi imetamatika rasmi huku akitoa ahadi ya kufikisha changamoto zilizokosa majibu ya papo kwa papo kuzifikisha katika mamlaka husika ili kupatiwa ufumbuzi.
Wananchi wa Jimbo la Ngara wakifurahia Jambo katika Ziara ya Mbunge wao Mhe. Ndaisaba George Ruhoro wakati akizungumza. |
Sehemu ya Wananchi wa Jimbo la Ngara wakifurahia Jambo katika Ziara ya Mbunge wao Mhe. Ndaisaba George Ruhoro wakati akizungumza. |
Pichani ni Mamia ya Wananchi wa Jimbo la Ngara katika Mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ndaisaba George Ruhoro alipokuwa katika Ziara ya Kata 22 Jimboni humo. |
إرسال تعليق