PAC : HATUJARIDHIKA NA KASI NDOGO YA MKANDARASI TONTAN KUPELEKA UMEME KWENYE VIJIJI 146 KAHAMA

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wananchi katika kijiji cha Ngongwa kata ya Ngongwa Wilayani Kahama, baada ya wajumbe wa Kamati ya ya Hesabu za Serikali kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Kahama

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Hesabu za Serikali (PAC) imefanya ziara ya kukagua miradi ya umeme Mkoani Shinyanga ambapo imeonesha kutoridhishwa na kasi ujenzi na usambazaji wa miundombinu ya umeme katika vijiji 146 Wilaya ya Kahama unaotekelezwa Kampuni ya Tontan Project Technology Co. Ltd Jv Group Six International kupitia Mradi wa Uwekezaji wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili(REA III awamu ya pili).

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ngongwa kata ya Ngongwa Wilayani Kahama, baada ya wajumbe wa Kamati ya ya Hesabu za Serikali kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Kahama, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Japhet Hasunga amesema kamati hiyo imeona mradi wa usambazaji umeme vijijini umecheleweshwa Kahama.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wananchi katika kijiji cha Ngongwa kata ya Ngongwa Wilayani Kahama.

Jambo ambalo tumeliona sisi hapa ni kwamba huu mradi umecheleweshwa na wananchi yale malengo yaliyokusudiwa bado hayajafikiwa. Sisi tutapima thamani ya fedha zaidi ya Bilioni 46 ambazo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kwa ajili ya Wilaya ya Kahama kwa ajili ya umeme pale ambapo wananchi wale ambao tulitarajia waunganishiwe umeme watakuwa na umeme, wananchi wanataka umeme. Kwa hiyo sisi kama kamati tutaenda kulisimamia”,amesema Hasunga.

Aidha amesema Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuanzia Mei 2,2024 na kuendelea itaenda kwa wananchi wa Kahama kuangalia kama wameunganishiwa umeme, na ndipo itakapotathmini na kupima kwamba thamani ya fedha ya zilizotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wilayani Kahama zimefanya kazi iliyokusudiwa, kama wananchi watakuwa hawajaunganishiwa umeme basi watamwambia kuwa fedha hizo zimetupwa.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Uwekezaji wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili mkoani Shinyanga, Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu amesema mkoa wa Shinyanga una jumla ya vijiji 509 ambapo vijiji 262 vimepatiwa huduma ya umeme ambapo kwa upande wa Wilaya ya Kahama yenye vijiji 146 ambapo vijiji pekee 63 vimepatiwa umeme bado vijiji 83.
Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu

Ameeleza kuwa, Mradi wa REA III awamu pili Wilayani Kahama unatekelezwa na Mkandarasi Tontan Project Technology Co. Ltd Jv Group Six International ambaye mshauri ni Mercados Aries International uliosainiwa Oktoba 29,2021 na kuanza kutekelezwa Februari 14,2022 ukitarajiwa kukamilika Aprili 30,2024 unatekelezwa kwa gharama ya shilingi 46,092,316,042.58/=.

Hata hivyo, Mkaguzi Mkuu wa Nje Wizara ya Nishati, Nyamisi Bituro amesema Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini kuwepo kasi ndogo ya ujenzi na usambazaji wa miundombinu ya umeme katika vijiji 146 Wilaya ya Kahama katika Mkataba wa REA na Kampuni ya Tontan Project Technology Co. Ltd Jv Group Six International kwa ajili ya ujenzi na usambazaji wa miundombinu, uwekaji wa transfoma pamoja na uunganishwaji umeme wa wateja (REA III awamu ya pili) kwa vijiji vya wilaya ya Kahama kwa kiasi. cha shilingi 46,092,316,042.58/= baada ya marejeo ya kuongeza mawanda ya wigo wa kazi.
Ukaguzi ulibaini uwepo wa marejeo ya kipindi cha kumalizika kwa mktaba ambapo muda wa mkataba uliongezwa kwa miezi minne hadi Desemba 31,2023 na kisha kurejewa tena kwa kipindi cha miezi minne hadi Aprili 30,2024”,amesema Bituro.

Hata hivyo, uhakiki wa ripoti za utekelezaji wa miradi uliofanywa mwezi Machi 2024 pamoja na uhakiki wa mradi ulibaini bado kuna kasi ndogo ya ukamilishwaji wa mradi ambaopo mradi umefikia 61.46% ikiwa umebaki mwezi mmoja tu wa kufikia ukomo wa mkataba. Hali hii inapelekea kuwanyima fursa wakazi wa vijiji vya wilaya ya Kahama ya kunufaika na nishati hii muhimu ya umeme kwa wakati”,ameongeza Bituro.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Balozi Meja Jenerali (Mstaafu) Jacob Kingu amesema REA  itahakikishia inasimamia kuchukua hatua za kisheria kwa Mkandarasi Tontan ili kuhakikisha anatekeleza mradi ndani ya muda uliopangwa.

Kuhusu Mkandarasi tutashughulika naye kuanzia baada ya kikao hiki kuhakikisha kwamba anaweka mambo yake sawa, asiwe mtu wa kunyoshewa vidole na yeye yupo hapa anasikia na mkataba unasimama Aprili 30,2024 na ndiyo maana REA imemuandikia Notisi lakini pamoja na hayo tu, tunataka wananchi wapate umeme, kwa hiyo ni kazi kazi atimize mradi katika muda uliopangwa", amesema.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amesema kucheleweshwa kukamilika kwa mradi huo kunakotokana na kazi za Mkandarasi kudorora kunasababisha viongozi wa siasa na serikali kuchonganishwa na wananchi kutokana na ahadi za mara kwa mara juu ya upelekaji umeme kwa wananchi.

Wananchi wanataka umeme na wanaona viongozi wanawadanganya kuwapa umeme wakati changamoto iliyopo ni Mkandarasi hana uwezo wa kukamilisha kazi kwa wakati, amekuwa akiongezwa muda wa kukamilisha kazi lakini hamalizi matokeo yake viongozi wanakosanishwa na Mkandarasi, viongozi wanaonekana wanasema uongo kwamba umeme utawafikia wananchi”,ameongeza Mhe. Mhita.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tontan Project Technology Co. Ltd Jv Group Six International, bw. John Zheng amesema miongoni mwa changamoto zinazosababisha wasikamilishe mradi kuwa ni ucheleweshaji wa vifaa kutoka kwa mzabuni na wizi wa vifaa katika eneo la mradi lakini watajitahidi kuhakikisha wanakamilisha mradi ndani ya muda uliopangwa ili wananchi waanze kunufaika na nishati ya umeme.

Nao wananchi akiwemo Thomas Welelo na Nshoma John wameiomba serikali jitihada za kumhamasisha Mkandarasi aongeze kasi ya kusambaza umeme vijijini.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wananchi katika kijiji cha Ngongwa kata ya Ngongwa Wilayani Kahama, baada ya wajumbe wa Kamati ya ya Hesabu za Serikali kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Kahama. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Balozi Meja Jenerali (Mstaafu) Jacob Kingu
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wananchi katika kijiji cha Ngongwa kata ya Ngongwa Wilayani Kahama, baada ya wajumbe wa Kamati ya ya Hesabu za Serikali kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Kahama.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Balozi Meja Jenerali (Mstaafu) Jacob Kingu akizungumza wakati wajumbe wa Kamati ya ya Hesabu za Serikali walipofika katika kata ya Ngongwa Wilayani Kahama kukagua miradi ya umeme 

Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu akizungumza wakati wajumbe wa Kamati ya ya Hesabu za Serikali walipofika katika kata ya Ngongwa Wilayani Kahama kukagua miradi ya umeme 

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wajumbe wa Kamati ya ya Hesabu za Serikali walipofika katika kata ya Ngongwa Wilayani Kahama kukagua miradi ya umeme 

Mkaguzi Mkuu wa Nje Wizara ya Nishati, Nyamisi Bituro akizungumza wakati wajumbe wa Kamati ya ya Hesabu za Serikali walipofika katika kata ya Ngongwa Wilayani Kahama kukagua miradi ya umeme 
Mkaguzi Mkuu wa Nje Wizara ya Nishati, Nyamisi Bituro akizungumza wakati wajumbe wa Kamati ya ya Hesabu za Serikali walipofika katika kata ya Ngongwa Wilayani Kahama kukagua miradi ya umeme 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tontan Project Technology Co. Ltd Jv Group Six International, bw. John Zheng akizungumza wakati wajumbe wa Kamati ya ya Hesabu za Serikali walipofika katika kata ya Ngongwa Wilayani Kahama kukagua miradi ya umeme 

Wananchi wakifuatilia kikao cha wajumbe wa Kamati ya ya Hesabu za Serikali waliofika katika kata ya Ngongwa Wilayani Kahama kukagua miradi ya umeme 

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA