MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Denis Londo ameongoza kikao cha kamati hiyo cha kupokea na kujadili taarifa ya Mkoa wa Tanga ya utekelezaji wa mpango wa bajeti fungu 86, Mkoa wa Simiyu fungu 47 na Ruvuma fungu 82 kwa mwaka 2023/24 kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Februari 2024 na mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka 2024/25.
Aidha Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe Justine Nyamoga aliongoza kikao hicho cha kupokea na kujadili taarifa ya Mkoa wa Morogoro ya utekelezaji wa mpango wa bajeti fungu 79 kwa mwaka wa 2023/24 kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Februari 2024 na mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka 2024/25.
Vikao hivyo vimehudhuriwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Dkt Festo Dugange, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Sospeter Mtwale, Wakuu wa Mikoa yote minne na watendaji kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
إرسال تعليق