WANATEMEKE WAJIPANGA KUHUISHA FUKWE KWA AJILI YA KUFURAHI


 

Ni sehemu Maarufu inayojulikana kwa jina la Kijiji cha Wavuvi eneo la Kurasini wilayani Temeke  ambapo kuna ufukwe mzuri wa bahari ambao kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwa ni pamoja na uvuvi, biashara ndogo ndogo na kutupia taka kutoka majumbani  pamepelekea kuwa kero na kusababisha wakazi wa Temeke na maeneo ya jirani kukosa eneo la kufurahi.


Kwa kuona umuhimu huo na shauku ya kuwa na sehemu ya ufukwe Taasisi zisizo za kiserikali ikiwa ni pamoja na TCCI, Mazingira Plus na Sanamare kwa kushirikiana na asasi nyingine zisizo za kiserikali kama HUDEFO, ETE, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mazingira TV, Ofisi ya Mtaa wa Kurasini, wakazi wa eneo la ufukwe na wadau mbalimbali wameungana kwa pamoja kufanya usafi katika eneo hilo ili hapo baadaye lianze kutumika kama sehemu ya watu kufurahi na kupumzika.

 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau mbalimbali wa mazingira wamefurahishwa na hatua hiyo ya kusafisha eneo hilo la fukwe na kuwaomba wavuvi, wafanyabiashara na wakazi wa maeneo hayo kuacha kutupa taka na kusema jukumu la kuweka safi eneo hilo sio lazima Serikali ila wananchi pia wanaweza na kuhimiza kuwa eneo hilo panatakiwa kuwa na Choo ili kuepuka magonjwa ya mlipuko kwa kuwa mpaka sasa watu wanaofanya shughuli mbalimbali wanajisaidia vichakani.

Wakati huo huo ETE walishiriki katika kufanya usafi eneo hilo kwa lengo la kuweka mazingira safi lakini pia kutumia Dijitali kuyasemea mazingira ambayo hayawezi kujisemea yenyewe, kwa Hashtag #ETEMazingiraKidijidali kwa kutumia mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali ya mtandaoni.














Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA