Pikipiki ya Mbabe wa Mauzo Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe Mkoani Geita
Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi (kushoto) akimkabidhi Plate Number Mbabe wa Mauzo Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe Mkoani Geita leo Ijumaa Machi 8,2024 katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wanawake wanaofanya kazi katika Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kukabidhi zawadi ya Pikipiki aina ya Boxer kwa mshindi wa shindano la Mbabe wa Mauzo ‘CRDB Sales Champions League’ Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe mkoani Geita aliyefungua akaunti zaidi ya 300 mwezi Januari 2024.
Hafla fupi ya makabidhiano ya Pikipiki ikiongozwa na Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddy imefanyika leo Ijumaa Machi 8,2024 katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga ikishuhudiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana wakati wanawake ulimwenguni kote wakisherehekea siku ya Wanawake Duniani.
Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana amesema shindano la mbabe wa mauzo linaendeshwa na benki ya CRDB kwa Wafanyakazi wa kujitolea ‘Freelancers’ walio chini ya Mawakala wa Benki ya CRDB lakini pia kwa Mawakala (Team Leaders) pamoja na wafanya kazi kwa benki ya CRDB.
“Kupitia shindano hili la Mbabe wa mauzo linalofanyika ndani ya miezi mine, zawadi ambazo ni pikipiki, bajaji, fedha taslimu zinatolewa kila mwezi kwa kila kanda na kwa mshindi wa jumla atapatiwa gari. Leo tunamkabidhi pikipiki aina ya Boxer ndugu Philbert Vedasto Baigana (Mbabe wa mauzo kwa mwezi Januari 2024) kutoka Runzewe Geita ambaye amefungua akaunti 350 na zina pesa”,amesema Wagana.
Kwa upande wake, Mbabe wa mauzo, Philbert Vedasto Baigana ambaye ameambatana na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Runzewe, Salum Ahmad Makwaya ameishukuru Benki ya CRDB kwa kumpatia zawadi ya Pikipiki akisema hakuamini kama angeibuka mshindi wa shindano la Mbabe wa mauzo.http://
Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddy (kushoto) akimkabidhi Plate Number Mbabe wa Mauzo Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe Mkoani Geita leo Ijumaa Machi 8,2024 katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi (kushoto) akimkabidhi Tisheti Mbabe wa Mauzo Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe Mkoani Geita leo Ijumaa Machi 8,2024 katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga.

Mbabe wa Mauzo Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe Mkoani Geita akiwa amepanda pikipiki aliyopewa zawadi ya kuongoza kufungua akaunti nyingi za benki kwa mwezi Januari ,2024

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kushoto) akimpongeza Mbabe wa Mauzo Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe Mkoani Geita
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa mbabe wa mauzo Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe Mkoani Geita
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa mbabe wa mauzo Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe Mkoani Geita
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa mbabe wa mauzo Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe Mkoani Geita
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Runzewe, Salum Ahmad Makwaya akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa mbabe wa mauzo Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe Mkoani Geita
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa mbabe wa mauzo Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe Mkoani Geita
Pikipiki ya Mbabe wa Mauzo Philbert Vedasto Baigana kutoka Runzewe Mkoani Geita
Wanawake wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani

إرسال تعليق