Katika jitihada zake za kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kidijitali nchini, Benki ya CRDB ilizindua msimu wa tatu wa kampeni ya ‘Benki ni SimBanking’ na kutenga jumla ya zawadi zenye thamani ya Shilingi milioni 470 kwa wateja wake mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, wakati wa kutangaza washindi wa droo ya mwezi wa pili wa kampeni hiyo, Meneja Mwandamizi wa Huduma za Kidigitali wa Benki ya CRDB, Mangire Kibanda amesema lengo la kampeni hiyo ni kujenga utamaduni wa matumizi ya kidijitali katika huduma za kifedha ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuondokana na matumizi ya fedha taslimu na kuwasihi wateja kuendelea kufanya miamala kupitia 'SimBanking' sababu inalipa.
Washindi wa awamu ya kwanza wa kampeni ya Benki ni SimBanking Miamala Inalipa ni Rahma Kyalumbika wa Dar es salaam, na Kibwana Killongo (kutoka Kibaha, Pwani) ambao kila mmoja ameshinda pikipiki huku Adamu Rashid (kutikea Chanika, Dar es salaam) akiibuka mshindi wa Bajaji kwa mwezi wa pili. Vyombo vyote hivi vitawekewa mafuta 'full tank' na kukatiwa bima kubwa.
Pamoja na zawadi hizi Benki hiyo pia imetenga kiasi cha Shilingi milioni 200 zitakazotolewa kupitia Tembo Points ambazo mteja atakuwa akikusanya kila anapofanya muamala. Wateja wataweza kubadili Tembo Points zao kuwa fedha na kuzitumia kulipia huduma au bidhaa. Pia zawadi za kompyuta mpakato kufikia 10 kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu, zawadi za simu janja, pamoja na fedha taslimu.
Meneja Mwandamizi Huduma za Kidigitali wa Benki ya CRDB, Mangile Kibanda (kulia) akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya msimu wa tatu wa kampeni ya ‘Benki ni SimBanking’ iliyofanyika katika makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Daress salaam. Katika droo hiyo, Washindi watatu walipatikana ambapo Wawili wamejishndia Pikipiki moja kila mmoja na Mwingine ameshinda Bajaj. Wengine pichani ni Afisa Masoko wa Benki ya CRDB, Salim Salim (kushoto) pamoja na Afisa wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Clara Chacha.
Afisa Masoko wa Benki ya CRDB, Salim Salim akifafanua jambo wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya msimu wa tatu wa kampeni ya ‘Benki ni SimBanking’ iliyofanyika katika makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Daress salaam. Wengine pichani ni Meneja Mwandamizi Huduma za Kidigitali wa Benki ya CRDB, Mangile Kibanda (kulia) na Katikati ni Afisa wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Clara Chacha.
إرسال تعليق