Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Ndg Jumanne Wambura Wagana amekabidhi madawati 50 kwa mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Elibariki Bajuta ikiwa ni mwendelezo wa benki hiyo ya CRDB katika kutekeleza sera yake ya uwekezaji kwa jamii lakini kuunga mkono jitihada za Serikali kwenye sekta ya elimu wilayani Urambo.
Akipokea Madawati hayo Aprili 4,2024, Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Elibariki Bajuta ambaye aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Urambo , Wakuu wa Idara wa Halmashauri pamoja na viongozi wengine ameishukuru sana Benki ya CRDB kwa msaada huo mkubwa na kuahidi kuendelea kuwapa mashirikiano makubwa zaidi kibiashara.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana (kushoto) akimkabidhi madawati Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mh. Eribariki Bajuta.
إرسال تعليق