Na, Mwandishi wetu - Arusha.
Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini Tanzania, taarifa iliyotufikia hivi punde ni kuwa mvua hiyo imesababisha mafuriko katika Kata ya Kisongo Wilaya ya Arumeru Jijini Arusha.
Kwa taarifa za awali mafuriko hayo yamesomba magari na kuhatarisha maisha wa wakaazi wa maeneo hayo, kusimama kwa shughuli mbalimbali za uzalishaji katika maeneo yaliyokubwa na mafuriko hayo jijini humo.
Mpaka sasa hakuna kauli yoyote ya serikali juu ya Mafuriko hayo.
إرسال تعليق