Mwanafunzi mmoja amepoteza maisha na saba hawajulikani walipo baada ya gari la shule ya Msingi Ghati Memorial, iliyopo Mkoani Arusha, kuanguka kwenye korongo linalopitisha maji katika mitaa ya dampo Sinoni, Kata ya Muriet huku chanzo kikidaiwa kuwa ni dereva wa gari hilo kushindwa kulidhibiti, kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Arusha, Osward Mawanjejele amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwa taarifa za awali ni kwamba gari hilo lilikuwa na watoto 11 na walimu wawili.
“Niko kwenye msafara wa Rais kwa ajili ya tukio la maadhimisho ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine, lakini kikosi hadi sasa wananiambia wameokoa watoto wanne na walimu wawili,bado wanaendelea kufuatilia wengine wanaosemekana walikuwepo kwenye hilo gari,” amesema.
Amesema kikosi chake kimeelekeza nguvu katika mto Themi ambapo korongo hilo linamwaga maji yake, ili kuona namna ya kuwaokoa watoto wengine wanaodaiwa walikuwepo ndani ya gari hilo
إرسال تعليق