NMB YAZINDUA KAMPENI YA UMEBIMA? KAHAMA - KANDA YA MAGHARIBI

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Benki ya NMB imezindua kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga - Kanda ya Magharibi kwa lengo la kuhamasisha Watanzania kukata Bima ili kulinda shughuli zao ikiwemo biashara pindi wanapopatwa na majanga mbalimbali yakiwemo ya moto, mafuriko na ajali zinazoweza kusababisha madhara na kusababisha kuyumba kiuchumi.

Uzinduzi huo uliokwenda sanjari na utoaji elimu na ushauri kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kukata Bima umefanyika leo Jumamosi Aprili 20,2024 katika Kituo cha Mabasi cha CDT Mjini Kahama.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio amesema lengo la Kampeni ya Umebima ni kutoa elimu ya masuala ya bima, kutoa ushauri pamoja na kuuza bima mbalimbali ikiwemo Bima ya Faraja inayolenga zaidi kutoa mafao ya pole kwa mwananchi anapopatwa na changamoto ya msiba au ulemavu ambapo mteja anajiunga kwa Shilingi 200/= na anapata fao kuanzia Sh.milioni 1 hadi 6.

“Ndugu zangu hivi karibuni mmekuwa mkishuhudia majanga ya moto, mafuriko na ajali mbalimbali, hivyo ni vyema ukawa na bima ili unapopatwa na majanga usipate hasara na kuepuka kuyumba kiuchumi. Njoo ukate bima kwa ajili yako na mali zako. NMB inashirikiana na kampuni mbalimbali za utoaji bima”,amesema Urio.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha amesema Kampeni ya Umebima ni mwendelezo wa kampeni ya Umebima katika Kanda mbalimbali nchini na kwamba wameamua kuzindua Kampeni ya Umebima Wilayani Kahama mkoani Shinyanga katika Kanda ya Magharibi kutokana na kwamba Kahama ni mji unaokua kwa kasi, una mwingiliano mkubwa wa watu lakini pia kuna wateja wengi wa NMB.

“Tunatoa elimu na ushauri kuhusu bima na kuuza bima ili kukabiliana na majanga yanapotokea., tunataka watu wote tuwafikie wapate bima ili kujikinga na hasara zitokanazo na majanga kwa kutoa fidia. Piatuna bima ya maisha, vyombo vya usafiri, bima kwa Wakulima na Wafugaji”,amesema Chacha.

Nao baadhi ya wafanyabiashara na wananchi waliofanikiwa kufikiwa na Benki ya NMB na kuwapatia elimu ya bima akiwemo Isaya Kisindo, Baningwa Charles na Moses Masasi wameishukuru Benki ya NMB kwa kupatia elimu ya bima na kuahidi kukata bima ili wao na mali zao ziwe salama na kwamba watahamasisha pia wananchi wengine wakate bima.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Aprili 20,2024 katika Stendi ya Mabasi CDT Mjini Kahama . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kahama, Said Pharseko akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Mabango wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima 
Mabango wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima  
Mabango wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima 
Wakazi wa Kahama wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama

Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama

Wakazi wa Kahama wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio (kushoto) akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Moses Masasi wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Mfanyabiashara Moses Masasi akihamasisha wananchi kukata bima wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Moses Masasi wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio (kushoto) akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Isaya Kisindo wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha (kushoto) akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Isaya Kisindo wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Mfanyabiashara Borondo Chacha akiishukuru na kuipongeza Benki ya NMB kutoa elimu kwa wananchi kwani wengi hawajui faida ya bima
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Baningwa Charles  wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Viongozi wa Benki ya NMB wakipita mtaa kwa mtaa Mjini Kahama kutoa elimu na ushauri kuhusu Bima wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga

Muonekano sehemu ya eneo la uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Muonekano sehemu ya eneo la uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Muonekano sehemu ya eneo la uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA