WAITARA CUP YAENDELEA KUTIKISA JIMBONI

 

                
                       Na, Mwandishi wetu - Mara.

Mbunge wa jimbo la tarime vijijini Mh Mwita Waitara ameshuhudia  michezo inayo endelea jimboni hapo leo ikiwa ni muendelezo wa ligi ya Waitara Cup ,ameweza kufika viwanja vya shule ya sekondari manga na shuhudia mchezo baina ya Komaswa Fc Na Bumera Fc.


Mbunge Witara Amewaeleza wazi wachezaji hao kuendela kuonyesha juhudi kwani pale hapo tu kwenye kucheza pia wakumbuke kuna kitu wana kipigania


‘’Nimekuja hapa kuagalia michezo hii pia nimefurahi sana kuona michezo inaendela vizuri maana hapa tumewekeza ko mnapo cheza kumbukeni kuwa kipo kitu mnakipigania na mnajua tumesha tangaza zawadi ko ni vizuri wasimamizi wa michezo hii wawambie ukweli wachezaji wajue kinacho piganiganiwa ni nini’’ Amesema Waitara 


Pia Mhe. Waitara amewataka waheshimiwa madiwani kuendelea kusaidia michezo hiyo inafanikiwa pia hata kama kuna wadau wa michezo basi wasisite kusaidia kuhakikisha timu zinafika uwanjani.


Hata hivyo mchezo huo umemalizika kwa 0-1 Komaswa Fc Na Bumera Fc, ikumbukwe kuwa mashindano hayo yanayoendelea yatakuwa na motisha ya zawadi kedekede kwa mchezaji bora, mfungaji bora na golikipa bora.






Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA