KAMATI YA BAJETI YAITAKA SERIKALI KUJENGA MAABARA ZA TEHAMA KILA SHULE


OR-TAMISEMI

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Oran Njeza ameiagiza Ofisi ya Rais- TAMISEMI kuhakikisha inajenga maabara za TEHAMA katika kila shule ili wanafunzi  wapate ujuzi  kwa lengo la kukabiliana  na mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani.

Ameyasema hayo leo Mei 21,2024 kwenye kikao cha kujengewa uwezo  wajumbe wa kamati hiyo kuhusu ufundishaji mubashara uliofanyika katika darasa janja katika Shule ya Sekondari Dodoma jijini Dodoma.
Mhe. Njeza amesema TEHAMA ndiyo inayojenga dunia kwa sasa hivyo ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kila shule inayojengwa inakuwa na maabara za TEHAMA na kuhakikisha zinaongezeka
kutoka maabara 3 hadi nne.


Ameitaka Serikali  kuhakikisha kila shule inakuwa na  maabara ya TEHAMA  ili  wanafunzi  wakitoka shuleni wawe na elimu ya kutosha  ya masuala ya TEHAMA na kuleta mabadiliko  katika kujifunza na kufundishia

Aidha Kamati imeridhishwa na matumizi ya madarasa janja kwa ajili ya kujifunzia na kufundishia ambapo kwa leo wameweza kuona matumizi ya TEHAMA yanavyoweza kufundisha shule ya Sekondari Dodoma, Dr Samia,Kibaha iliyopo Mkoa wa Pwani na shule ya sekondari ya Mtakuja ya Zanzibar.


Naye Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Zainab Katimba ameieleza Kamati ya Bunge ya Bajeti kuwa Serikali imepanua wigo wa matumizi ya TEHAMA  katika kufundisha wanafunzi ili kupunguza changamoto  ya upungufu wa walimu nchini.Zipo njia nyingi za kukabiliana na changamoto ya Walimu,njia hizo ni pamoja na kuendelea kuajiri walimu na kutumia TEHAMA katika kufundisha na kujifunza.


Vilevile ameileza kamati kuwa ni maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa  kuhakikisha kila Halmashauri inatenga fedha za mapato ya ndani ya kuanza kujenga  madarasa janja  pamoja na ngazi ya Mikoa  kujenga kituo kimoja  cha TEHAMA katika ngazi ya Mkoa.
 







 
 
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA