Na, Mwandishi wetu - Dodoma.
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo katika mwaka wa fedha 2023/2024 inaendelea na taratibu za kukamilisha ujenzi wa soko la kimkakati lililokuwa chini ya mradi wa DASIP lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Sirari) katika kijiji cha Remagwe ikiwa ni baada ya kutangazwa Zabuni Mwezi Desemba, 2023 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa soko hilona mpaka sasa mzabuni amekwisha patikana.
Majibu hayo ya serikali yametolewa Mei 29, 2024 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tarime vijijini Mheshimiwa Mwita Waitara alilotaka kujua "Je? lini soko la Remagwe - Siari litajengwa?" ambapo pamoja na mambo mengine amesema mpaka kufikia sasa zabuni kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo ipo katika hatua ya upekuzi.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Silinde amebainisha mpango mkakati wa serikali ni kukamilisha ujenzi huo katika bajeti ya ya wizara kwa mwaka wa fedha 2024/25 ili kuwawezesha wananchi kuendeleza biashara ya mazao ya mchele na mahindi katika maeneo ya mpakani.
"Wizara itaendelea kukamilisha ujenzi wa soko hilo katika mwaka wa fedha 2024/2025, Aidha, Kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo utawezesha kuendeleza biashara ya mazao ya mchele na mahindi katika maeneo ya mpakani hususan nchi ya Kenya." Amesema Naibu Waziri Silinde
إرسال تعليق