DODOMA.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg. Abdulmajid Nsekela, Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 21 Juni, 2024.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia ameipongeza Benki hiyo kwa namna ambavyo inashirikiana vizuri na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na jinsi ambavyo imekuwa ikijihusisha na mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi.
إرسال تعليق