Kupitia taarifa iliyototewa na moja ya chombo cha habari nchini Tanzania kuhusu gari la kifahari aina ya Toyota Land Cruiser V8 kutumika kusafirisha wahamiaji haramu kutoka Ethiopia limezidi kushika kasi zaidi baada ya gari hilo kuhsishwa kuwa ni la Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Fakih Nyakunga ya kukiri kuwepo kwa tukio hilo.
Pamoja na mambo mengine sakata hilo limeibuka na sura mpya na kuibua hisia mbaya, maswali na fumbo kwa umma ya kutaka kujua undani wa taarifa hiyo ambayo ili ahidiwa kutolewa ufafanuzi wa kina na mpaka sasa Fichuzi News Blog ikitoa chapisho hili bado kimya kimezidi kutanda na kuacha maswali katika vichwa vya wengi.
Ikumbukwe kuwa Taarifa iliyotolewa na Chombo cha Mwananchi digital ilieeza kuwa "Wimbi la magari ya kifahari kutumika kusafirisha wahamiaji haramu kutoka Ethiopia, linazidi kushika kasi nchini na safari hii gari linalodaiwa kuwa la Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, likikamatwa na wahamiaji haramu saba.
Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser V8 lilikamatwa jana saa 2:00 asubuhi katika hoteli moja iliyopo Njiapanda ya Himo, Barabara ya Moshi-Dar es Salaam Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, lakini wakati likikamatwa, mbunge huyo hakuwemo ndani ya gari.
Alipotafutwa na Mwananchi, Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Fakih Nyakunga amekiri kuwepo kwa tukio hilo na ameomba apewe muda mpaka leo Jumatano, ndiyo alizungumzie suala hilo kwa kina baada ya kukusanya taarifa kamili.
“Ni kweli kuna tukio kama hilo. Naomba tuonane kesho (leo) nikishaweka mambo vizuri. Siwezi kuzungumza hapa kwa sasa. Kuna mambo hayajakaa sawa ila kweli hilo tukio (la kukamatwa kwa gari la Mbunge) lipo,” amesema Kamanda Nyakunga.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa hazikuzaa matunda, kila alipopigiwa simu alijibu yuko kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi."
Je ni yapi maoni yako kuhusiana na sakata hili?......
إرسال تعليق