MSONDE:TUMIENI MFUMO KUSHUGHULIKIA UHAMISHO WA WATUMISHI

 


OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde amewataka watendaji wa Hamshauri nchini kushughulikia uhamisho wa walimu na watumishi wengine kwa kutumia mfumo uliowekwa ili kuondoa sitofahamu zinazojitokeza.

Dkt. Msonde ametoa maelekezo hayo kwenye kikao kazi cha majumuisho ya ziara ya katika mkoa wa Tabora kilichowakutanisha walimu,walimu wakuu,wakuu wa shule,Maofisa Elimu na wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa huo kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Mihayo Manispaa ya Tabora.

“Siku zote kuwa makini kuona kwenye mfumo tunapitisha nini kwasababu watu wameomba uhamisho ni lazima tuwapitishie ili mwenye mamlaka ya kuidhinisha uhamisho akiona haitahili yeye atakataa lakini sisi tuwapitishie kulingana na maombi yao, ” amesema

Dkt. Msonde amesisitiza kuwa endapo mkurugenzi atakuwa amebanwa na shughuli zingine na kushindwa kuingia kwenye mfumo anapaswa kukasimu mamlaka kwa mtu mwingine ili kuhakikisha maombi hayakai kwa muda mrefu na kuwaacha watumishi wakilalamika.

Akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Tabora,  Grace  Quintine ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ameahidi kufanyia kazi  maelekezo hayo na kuyasimamia  ili kuwe na ufanisi katika sekta ya Elimu katika mkoani humo. 




 

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA