UBIA WA TWIGA MINERALS NA BARRICK WAZIDI KULETA MANUFAA, YATOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 53.5 KWA SERIKALI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan akipokea hundi ya gawio kutoka kwa Meneja wa Barrick nchini,Melkiory Ngido (Kulia)
Baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali katika hafla hiyo
Viongozi wa taasisi mbalimbali na wageni waalikwa katika hafla hiyo.


Katika kudhihirisha kuwa ubia kati ya kampuni ya Barrick Corporation na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals unaendelea kunufaisha pande zote mbili ,Twiga imetoa gawio la bilioni 53,482,072,393 kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutunukiwa tuzo ya nafasi ya pili kwa kutoa gawio kubwa mwaka huu.

Hundi ya gawio hilo (Dummy cheque) ilikabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido, katika hafla ya Serikali kupokea gawio kwenye makampuni ambayo ina hisa nayo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam

Mwaka uliopita Twiga ilishika nafasi ya kwanza kutoa gawio kwa Serikali ya kiasi cha shilingi bilioni 84 katika mwaka wa fedha 2022/23.

Migodi iliyopo chini ya kampuni ya Barrick na Twiga Minerals nchini ni North Mara , Bulyanhulu na Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa.

Kampuni ya Twiga mbali na kutoa gawio nono kwa Serikali imekuwa ikichangia pato la serikali kupitia malipo ya tozo mbalimbali katika halmashauri zinazotozwa katika maeneo yenye shughuli za migodi yake sambamba na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa kupitia kodi, ushuru, magawio, mishahara na malipo kwa wazabuni wa ndani.
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA