"WAAJIRI TIMIZENI WAJIBU WENU, SERIKALI ILIPE MADENI YA WATUMISHI - KATIBU TALGWU



Chama cha wafanyakazi wa serikali za Mitaa Tanzania Mkoa wa Dodoma TALGWU kimeiomba Serikali likizo za Watumishi wasio Walimu ziwe zinagharamiwa na Ruzuku kutoka Serikali Kuu hasa kwa Halmashauri za Wilaya ambazo hazina mapato ya kutosha.


Maombi hayo yametolewa na Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Dodoma Ndg. Audaxs Stanslaus katika Mkutano wake na watumishi hao wa kada ya afya  tawi la Mvumi Mkoani Dodoma.


Aidha, ameiomba Serikali kulipa Madeni ya Mishahara kwa watumishi walioondolewa katika Utumishi wa Umma mwaka 2018 na baadae wakarudishwa kazini kwani hawakulipwa mishahara yao pindi walipokuwa wameondolewa Kazini ambapo katika Mkoa wa Dodoma wapo zaidi ya Watumishi 57.


Katika Hatua nyingine, Chama hicho kimetoa rai kwa waajiri wote wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanapandisha na kubadilisha vyeo watumishi kwa wakati.


"Hatua hiyo itaondoa uwezekano wa kuisababishia Serikali Madeni yasiyo ya lazima, Aidha watumishi wote wanahimizwa kujaza Taarifa zao kwenye mfumo wa Pepmis ili waweze kufikia Asilimia walizoelekezwa" amesema Katibu TALGWU.

Mfumo wa PEPMIS ni miongoni mwa jambo linalolalamikiwa na watumishi wengi na kusema kuwa umekuja wakati ambao sio sahihi kwa sababu mfumo huo umeingia katikati ya Msimu jambo ambalo linaweza kupelekea mtumishi kusomeka sehemu nyingine aliyosajiliwa na kuonekana ni mtoro Kazini na hata kupelekea kukosa fursa ya kupandishwa Vyeo.


   Jackson Chigelika ambaye ni Afisa Kilimo na Mifugo Kata ya Mvumi Makulu ameshauri kuwa ni vyema mifumo hiyo migeni iwe inaanza mapema na kuwepo na muda wa kutoa mafunzo walau kipindi cha Miezi mitatu ili kujiridhisha.

 





 

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA