KAMPUNI YA SWALA SOLUTION YAWAJENGEA NYUMBA WALIMU MSALALA


Nyumba ya walimu iliyojengwa na kampuni ya Swala
Wafanyakazi wa Swala Solution na walimu wa shule ya msingi Nyangaka wakifurahia uzinduzi wa nyumba ya walimu
Wafanyakazi wa Swala Solution na walimu wa shule ya msingi Nyangaka wakifurahia uzinduzi wa nyumba ya walimu
Mwakilishi wa kampuni ya Swala Solution, Raymond Warioba, akiongea katika hafla hiyo
Walimu wa shule ya msingi Nyangaka wakifurahi na kutoa zawadi kwa wageni katika hafla hiyo
Wafanyakazi wa Swala Solution wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Wanafunzi na wageni waalikwa katika hafla hiyo
Picha ya pamoja ya walimu na wafanyakazi wa Swala katika hafla hiyo

**

Kampuni ya Swala Solution, inayofanya kazi katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu, kupitia sera ya uwajibikaji kwa jamii imeunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha sekta ya elimu ambapo imejenga nyumba ya kisasa ya walimu katika shule ya msingi ya Nyangaka iliyopo katika wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.

Hafla ya kukabidhi nyumba hiyo ilihudhuriwa na walimu, wanafunzi,wafanyakazi wa Swala Solution na Wanakijiji wa kata ya Bugarama ambapo mgeni rasmi alkuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala ambaye aliwakilishwa na Afisa Mwandamizi wa Halmashauri hiyo, Najuka Sumeye.

Akiongea katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Najuka Sumeye , aliipongeza Kampuni ya Swala Solution kwa Kuunga mkono jitihada za Serikali katika Kuinua sekta ya elimu nchini ambapo imefanikisha kujenga nyumba za walimu katika shule ya Nyangaka.

"Walimu wetu katika shule hii walikuwa na changamoto ya nyumba za kuishi hali iliyosababisha kuishi mbali na eneo la shule,kupatikana kwa nyumba hizi kutapunguza changamoto hii na utachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufaulu wa Wanafunzi", alisema.


Kwa upande wake Mwakilishi wa kampuni ya Swala Solution, Raymond Warioba, alisema ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa umegharimu zaidi ya shilingi milioni 110 na ameshukuru uongozi wa shule ,kijiji pamoja na Kata ya Bugarama kwa ujumla kwa kutoa ushirikiano mzuri kufanikisha mradi huo.

"Kampuni yetu itaendelea kushirikiana na mgodi wa Bulyanhulu na Serikali Katika kuwaletea maendeleo wananchi wanaozunguka maeneo ya Mgodi ili wanufaike na uwekezaji katika sekta ya madini", alisisitiza Warionba.


Akizungumza kwa niaba ya Meneja Mahusino ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Marry Lupamba, alisema mgodi unao mkakati wa kushirikiana na makampuni yote yanayofanya kazi ndani ya Mgodi kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii kwa ajili ya Wananchi maeneo yanayozunguka mgodi huo.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA