SERIKALI YAJA NA MBINU YA JAMII KUKABILIANA NA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU

 


Na John I. Bera - Morogoro

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani (FAO) iko katika hatua ya mwisho ya kukamilisha machapisho ambayo yatatumia katika kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na  namna bora  ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu.

Akizungumza wakati wa Kikao kazi cha kuboresha machapisho hayo, Afisa Mhifadhi kutoka  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Isaac  Chamba amesema machapisho hayo yanakwenda kusaidia kupunguza madhara ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa jamii.

Amesema machapisho haya yanalenga kutoa elimu ambayo itaifikia jamii kwa lugha yepesi na kuwezesha wananchi walio maeneo mbalimbali yanayokabiliwa na wanyamapori wakali na waharibifu kupata uelewa wa hatua za kuchukua kuepuka madhara yanayosababishwa na wanyamapori wakali na waharibifu kwa kuchukua tahadhari.


Naye Mratibu wa programu hii ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu kutoka FAO ofisi ya Tanzania, Beatha Fabian amesema anategemea ushirikiano kutoka  kwa wadau na  Wizara  ili kutekeleza - lengo la kutatua changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu

Aidha, Amesema wamejipanga kuandaa mkakati wa namna ya kutoa elimu hiyo kwa jamii kwa urahisi zaidi  namna ya kukabiliana na changamoto ya migongano baina ya  binadamu na wanyamapori.


Programu hii ilianzishwa kufuatia mashirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika la Chakula Duniani (FAO) Ofisi ya Tanzania katika kudhibiti kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu.

Kikao hicho kimeshirikisha pia maafisa wanaoshughulikia masuala ya wanyamapori wakali na waharibifu kutoka Idara ya wanyamapori katika  kitengo cha wanyamapori wakali na waharibifu , Afisa kutoka kitengo cha habari na mawasiliano,Maafisa kutoka TAWA,TANAPA na TAWIRI
   


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA