AGNESS SULEIMAN KAHAMBA ASHINDA TUZO YA MWANAMKE MASHUHURI AFRIKA 2024

   

MWANAHARAKATI  wa masuala ya kijamii na Mwanamziki maarufu Tanzania  Agness Suleiman Kahamba amekabidhiwa tuzo yake kupitia taasisi yake ya Tupaze Sauti Foundation baada ya kutangazwa mshindi kipengele cha ‘Notable in community Development’ katika tuzo za ‘100 Most Notable Africans Awards’ zilizofanyika nchini Rwanda.

Hivi ndivyo inavyosadifu kwa mambo anayoyafanya Agness Kahamba, binti wa Kitanzania aliyejipatia umaarufu duniani na kupata tuzo kadhaa kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya ndani ya muda mfupi katika kutetea haki za wanawake, vijana na watoto.

Tangu mwaka 2018, Agness ambaye ni Mwasisi na Rais wa Tupaze Sauti Foundation (TSF), taasisi isiyo ya kiserikali (NGO) na Balozi wa Kutetea Unyanyasaji dhidi ya Watoto, ameshatwaa tuzo kadhaa ambazo zimemfanya kuwa miongoni mwa Watanzania waliopata umaarufu katika medani ya kimataifa.

Hivi karibuni, Agness alipata Tuzo ya Wanawake Maarufu Af- rika 2024 (Most Notable Women in Afrika 2024) katika masuala ya familia na maendeleo ya jamii. Tuzo hii imemfanya kuwa mmoja wa watu 100 mashuhuri barani Afrika.

Tuzo hii imekuja baada ya mwaka jana kupata tuzo ya mmoja ya watu 100 wa juu waanzilishi wa NGO. Alipata tuzo hiyo kwa kutetea na kuleta mabadiliko katika maisha ya watu kwenye masuala ya usawa wa jinsia, ukatili dhidi ya watoto, elimu, afya, uwezeshaji wanawake, haki za binadamu na maendeleo ya jamii. 

Tuzo hizo zilikuwa mwendelezo wa ile aliyoipata mwaka 2018 baada ya kushika nafasi ya 16 ya Tuzo ya Vijana 50 wa Tanzania wenye Ushawishi.
Mambo hayo hayakupatikana kwa urahisi bali kwa kazi kubwa na yenye kujituma katika yale aliyothubutu kuyafanya baada ya kuanzisha TPF mwaka 2008 kwa lengo la kupinga unyanyasaji wa kijinsia, ukatili dhidi ya wa- nawake na watoto na uwezeshaji kwa vijana.
-
“Malengo ya asasi yetu ni pamoja na elimu kwa jamii, kuwawezesha vijana kujitambua, ujasiriamali kwa wanawake na kutambua haki zao. Pia uhamasishaji katika kukabilinana na matukio ya dharura yakiwamo magonjwa ya mlipuko kama ilivyokuwa UVIKO- 19,” alibainisha katika mahojiano maalum na Nipashe Jumapili.

“Mimi ni mwanamke, mama, binti na kijana, hivyo niliona hayo maeneo ni ya muhimu kuyafanyia kazi kwa sababu ya- nanihusu kwa namna tofauti. Makundi haya ndiyo yenye shida katika jamii. Kwa serikali pekee ni vigumu kutatua shida za makundi hayo bila msaada wa wadau. Kwa hiyo niliona ni fursa kuanzisha asasi hii kuwezesha jamii kupaza sauti.

Agness alibainisha kwamba wanawake katika baadhi ya maeneo, hasa vijijini ambako mwamko wa elimu kwa mtoto wa kike ulichelewa, kumekuwa na dhana iliyojengeka kutokana na imani kwamba mwanamke anapoolewa hawezi kuachana na mume hadi kifo kitakapowatenganisha.
Hali hiyo, anasema imewafanya baadhi ya wanawake kuamini kuwa ni mwiko au dhambi kuachana na mume baada ya kufunga ndoa. Alisema kutoka- na na fikra hiyo, baadhi wanaogopa aibu ya kuonekana kuwa wameondoka kwa waume zao, hivyo wanalazimika kuvumilia hata wakipata vipigo, ulemavu wa kudumu hata kupoteza viungo.

“Kwa kweli katika hili la utetezi na elimu kwa wanawake dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, kwa kushirikiana na wadau wengine, tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Wanawake hivi sasa kwa sehemu kubwa wanatambua haki zao na kujik- ita katika uzalishaji na kumiliki mali,” alisema.

Licha ya wanawake, haki za mtoto hasa wa kike, alisema limekuwa la kipaumbele ili kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu na kuwaepusha na ndoa za utotoni, ukeketaji na unyago.

Kwa vijana, alisema lengo kubwa ni kuwafanya wajitambue na kupata maarifa ya kufanya kazi badala ya kuwa na fikra kwamba maendeleo yata- patikana kwa njia ya mkato au kufanya michezo ya kubashiri (betting).

“Baadhi ya vijana wamekuwa wakidanganyana kuwa illi kuwa na maisha mazuri lazima uende nje. Wengine wamwekuwa wakijiingiza katika vitendo vi- chafu kama ushoga ambavyo ni hatarishi kwa afya na maisha yao. Kupitia programu mbalim- bali, TSF tunawaelimisha kuhu- su stadi za kazi na maisha na kujitambua kuhusu maisha yao kwa ujumla,” alisisitiza.


MAFANIKIO

Tangu kuanza kwa TSF, Ag- ness alisema kumekuwa na mafanikio makubwa. Moja ya mafanikio hayo ni mapambano dhidi ya ukeketaji, ndoa za utotoni na unyago.

Kwa mujibu wa Agness, utekelezaji wa programu za asasi hiyo zilizofanyika katika mikoa minane nchini, ume- saidia kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na ku- pata elimu kuhusu haki zao. 

Pia alisema vijana wengi wamejitambua kuhusu maisha yao na mustakabali wao.

“Katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, vitendo vya unyago kwa watoto wa kike vi- likithiri pamoja na ndoa za utotoni. Wazazi walikuwa chanzo cha kushamiri kwa vitendo hivyo kwa tamaa ya kupata ma- hari wanapowaozesha na pia mila na desturi zao. Tulifanya kila juhudi na sasa hali ni tofauti na ilivyokuwa awali. Vitendo hivyo vimepungua kwa kiasi kikubwa.

“Tulifanya kampeni ya ku- tokomeza vitendo hivyo kwa kutembelea shule nane kutoa elimu kuhusu umuhimu wa elimu badala ya ndoa. Tulitoa elimu kwa wazazi kuhusu mad- hara ya unyago na ukeketaji kwa sababu wazazi walikuwa mstari wa mbele kwa ndoa za utotoni kutokana na tamaa ya fedha kwa kutoza mahari na wakati huo huo wanakatisha ndoto za mabinti za kuwa watu mashuhuri baada ya kupata elimu.

“Katika kampeni ile, tuliongozana na mkuu wa wilaya na ofisa elimu wa wilaya kutoa elimu kuhusu madhara ya ukeketaji, unyago na ndoa za uto- toni. Pia polisi walikuwapo na waliwaambia waziwazi wazazi kuwa yeyote atakayeendelea na vitendo hivyo atachukuliwa hatua. Kwa kweli hili lilileta matokeo chanya,” alisema.

Licha ya kufanikiwa huko, alisema kwa wale watoto wa kike waliokeketwa, walikuwa wakipelekwa kupimwa afya kwa sababu walikuwa waki- fanyiwa vitwendo hiyo kwa wembe au kisu kimoja, hali ambayo ni hatari kwa afya zao.
Aidha, Agness alisema baada ya kufanya kampeni hiyo, wali- rudi walayani humo kwa ajili ya ufuatiliaji na kutoa msaada kwa waathirika na kubaini kwamba kuna mabadiliko makubwa. Wa- toto wengi waliokuwa wame- olewa, wamerejeshwa shuleni kuendelea na masomo na wengine kupelekwa vyuo vya ufundi.

BADO CHANGAMOTO

Pamoja na mafanikio ya asasi yake na wadau wengine katika mapambano dhidi ya ukatili na unyanyasaji, dhidi ya wanawake na Watoto pamoja na vijana kujiingiza katika makundi maovu, Agness alisema bado kuna changamoto kutokana na sababu mbalimbali, likiwamo suala la haki za binadamu.

“Masuala kama haki za binadamu yamesababisha kuwapo kwa vikwazo katika kufanikisha mapambano dhidi ya mambo kama ya ushoga, ndoa za jinsia moja. Hapa hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa ikiwamo kutungwa kwa sheria,” alishauri.
ipate taarifa kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo kwa haraka,” anasisitiza.

TUZO CHACHU

Kuhusu tuzo hizo, Agness alisema zimekuwa kichocheo kwake katika kusonga mbele kwenye malengo aliyojiwekea kupitia asasi ya Tupaze Sauti.

“Tuzo hizi zimeniweka katika viwango vikubwa na kunifanya niendelee kufanya mambo makubwa katika jamii. Hii (tuzo) ya sasa ndiyo imenitambulisha kwa mchango wangu na kuwa miongoni mwa wanawake wanaojitoa kupigania haki za makundi maalum hasa wanawake, vijana na watoto".

Pia alisema tuzo hizo zimedhihirisha namna alivyojitoa katika kuwatetea watu wa makundi hayo maalum ambayo yamekuwa yakipitia changamoto mbalimbali.

Kwa mujibu wa Agness, wanawake kwa mfano, kwa miaka mingi wamekumbana na vitendo vya unyanyasaji hasa vipigo kutoka kwa waume zao na wengine kupata ulemavu wa kudumu.
Kutokana na hali hiyo, alisema TSF iliona ni vyema kujitosa na kuwatetea ili wajue haki zao na hatimaye kujikomboa dhidi ya ukatili na unyanyasaji huo.

“Katika hili, tunatoa elimu kwa wanawake ili kutambua  haki zao".

CHANZO - NIPASHE JUMAPILI
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA