Na, Mwandishi wetu kutoka - Dodoma.
Leo Agosti 2, 2024 umefanyika uchaguzi wa kumtafuta mrithi wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Harold Sungusia na hatimae matokeo ya kura yameamua Boniface Mwabukusi kushikilia kiti hicho.
Mwabukusi ambaye alionekana kuwa imara na jasiri wakati kampeni zake imeibua sura mpya baada ya kuibuka na kura 1,274 sawa na asilimia 57.4 dhidi ya wapinzani wake watano ambao ni Ibrahim Bendera, Emmanuel Muga, Sweetbert Nkuba, Revocutus Kuuli na Paul Kaunda.
Uchaguzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma huku matokeo yakitangazwa majira ya saa tano usiku katika hali isiyo ya kawaida sababu ikitajwa kuwa ni msiba wa mmoja wa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho ikapelekea muda kusogezwa mbele.
إرسال تعليق