Na, Mwandishi wetu - Dodoma.
Agosti 20, 2024 imeendelea kusikilizwa kesi ya watuhumiwa wa ubakaji na ulawaiti wa binti wa Yombo - Dovya wa Jijini Dar es Salaam katika kituo jumuishi cha utoaji haki Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Dodoma.
Shauri hilo lililosikiizwa kwa mara ya pili lililokuwa na dhima ya kusomwa kwa hoja za awali ambapo Mmoja kati ya mawakili watetezi wa shauri hilo wakili Meshaki Ngamando ameweka bayaya kwa kile kilichojiri na kuwa upande wa Jamhuri walikua na mashahidi watano.
"Kwa bahati mbaya tulianza muda ukiwa mbaya sana, tulianza saa nane mchana na kama mnavyoona kesi yenyewe ikiwa na watuhumiwa wanne tangia tumeanza kusoma hoja za awali kwahiyo tumechukua muda sana ndipo tukaanza hatua ya usikilizwaji ambapo yulibahatika kumsikiliza shahidi mmoja ambapo tumefikia hatua ya kumuuliza maswali" wakili Ngamando.
Ikumbukwe kuwa kutokana na unyeti wa jambo lenyewe shauri hilo limepangwa kusikilizwa kwa mfululizo wa siku tano huku likiteka hisia za wananchi wengi wakitaka hatua/ sheria madhubuti kuchukuliwa ili kukomesha matukio ya ukatili kwenye jamii.
Hata hivyo Fichuzi Blog itaendelea kukusogezea kwa karibu mwendelezo wa matukio ya kesi hiyo ambayo inaendelea katika Kituo Jumuishi cha Utoaji haki Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Dodoma.
إرسال تعليق