NA MWANDISHI WETU, KINONDONI.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni imemhukumu Fundi Umeme Bw. SAID NASIBU KILANGA adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya sh. Laki mbili (200,000) baada ya kukutwa na hatia katika kosa la kutoa rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1) (b) & (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 329 Rejeo la 2022.
Hukumu dhidi ya Bw. Said Nasibu Kilanga imetolewa Julai 31, 2024 kutokana na shauri la jinai namba 218/2023 lililokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mbele ya Hakimu Nabwike Mbaba, shauri ambalo liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wilaya ya Kinondoni Bw. Aidan Samali
Ilielezwa kuwa Mshtakiwa alifikishwa mahakamani hapo Septemba 5, 2023 kwa shtaka tajwa hapo juu ambapo mshtakiwa alitoa rushwa kiasi cha sh 50,000/= kwa Askari Polisi wa Kituo cha Polisi Mburahati Bw. Yusuph Nammohe ili amsaidie kumaliza tuhuma za wizi wa mtandaoni zilizokuwa zikimkabili kituoni hapo.
Mahakama katika hukumu yake imemkuta mshtakiwa na hatia na kumhukumu kifungo cha mwaka mmoja gerezani au kulipa faini ya sh. Laki mbili (200,000) ambapo mshtakiwa amelipa faini hiyo.
إرسال تعليق