JESHI LA POLISI KATAVI LAWATIA NGUVUNI WATUHUMIWA AKIWEMO TAPELI ALIYEJIFANYA MTUMISHI WA SERIKALI


Na, Jackso Gerald - Katavi.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi  lina mshikilia mtuhumiwa mmoja alie jifanya mtumishi wa serikali Afisa biashara katika Halimashauri ya Wilaya ya Mpimbwe  Mkoani humo.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 05,2024 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Davidi Mutasya amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo aliyejifanya mtumishi wa serikali kwa lengo la kuwaibia wananchi  kupitia cheo hicho.


Sambamba na hayo Mutasya amebainisha kuwa Jeshi hilo limefanikiwa  kuwafikisha  Mahakamani watuhumiwa 51 na kuhukumiwa vifungo mbalimbali.


Amesema watuhumiwa wawili walihukumiwa miaka 20 jela kwa kosa la kupatikana na nyara za serikali, mtuhumiwa  mmoja miaka mitano jela kwa kosa la wizi wa Mifugo alikadhalika watuhumiwa wengine kwa makosa yanayo landana na hayo.


Amebainisha kuwa kwa upande wa usalama barabarani  Jeshi la hilo limezuia ajali kwa kiasi kikubwa kutokana na jitihada mbalimbali zinazo endelea  ikiwemo utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali ya watumiaji  wa barabara.


Amesema katika kuimarisha usalama barabarani jeshi hilo limefanikiwa kuongeza nguvu na umakini katika ukaguzi wa Madereva wakati wa kiendesha vyombo vya moto na kufanikwa kukamata jumla ya makosa 2057 ambayo yalikuwa yanachangia ongezeko la ajali barabarani.


Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi lina toa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo viovu vya kihalifu  na kutoa taarifa  za uhalifu na wahalifu ili Jeshi hilo  liweze kuchukua hatua za kisheria na kuimarisha ulinzi na usalama katika jaamii.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA