JKT YAKANUSHA KUTOA AJIRA, MAFUNZO KUANZA KWA VIJANA WA KITANZANIA ILI KUJIAJIRI


Na, Mwandishi wetu - Dodoma.

JESHI la kujenga Taifa nchini JKT limesema linatoa mafunzo kwa Vijana wa kitanzania kwajili ya kujiajiri lakini halitoi ajira.

Kauli hiyo imebainishwa na Kaimu Mkuu wa  Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa JKT Juma Mrai leo Septemba 25,2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari  kuhusu kutoa wito kwa Vijana wa Kitanzania kujiunga na mafunzo ya kujitolea Kwa Mwaka 2024.

Pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa  Wananchi kujihadhari na matapeli ambao wamekuwa wakitumia fursa hiyo kudanganya watu kuwa Jeshi la JKT linatoa ajira na kuwatapeli wananchi.

"Jeshi la kujenga Taifa linapenda kuwataarifu Vijana watakaopata fursa hii kuwa Jeshi la kujenga Taifa halitoi ajira, pia halihusiki kuwatafutia ajira katika Asasi, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyo ya kiserikali, bali hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza mkataba wao na Jeshi la kujenga taifa." Amesema Kaimu Mkuu wa  Tawi la utawala Jeshi la kujenga Taifa JKT Juma Mrai 

" Sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo yanapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz"

Aidha Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawakaribisha vijana wote watakaopata fursa hiyo kujiunga na vijana wenzao ili kujengewa Uzalendo,Umoja kitaifa,Ukakamavu,Kufundishwa stadi za kazi,Stadi za Maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa lao.

Hata hivyo usaili wa vijana hao kujiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa kwa kujitolea utaanza tarehe 01 oktoba,2024 kwa mikoa yote Tanzania bara na visiwani,Vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya Jeshi kuanzia tarehe 01Novemba,2024 hadi 03 Novemba 2024.

"Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo,unaratibiwa na ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya ambako mwombaji anaishi"


JESHI la kujenga Taifa nchini JKT limesema linatoa mafunzo kwa Vijana wa kitanzania kwajili ya kujiajiri lakini halitoi ajira

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA