MELEKEZO YA RAIS SAMIA KWA WAFANYABIASHARA WALANGUZI, ATOA WITO HUU KWA WANANCHI NCHINI

 

Na Mwandishi wetu - Ruvuma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aamesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa wakulima wanapata faida kutokana na juhudi zao hii ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020-2025, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wakulima nchini Tanzania.


Dkt. samia ametoa wito huo leo Septemba 25, 2024 wakati alipotembelea kituo cha ununuzi wa mahindi kilichopo katika Soko Kuu Mbinga mjini Mkoani Ruvuma ambapo pamoja na mambo mengine alipata maelezo ya undani kuhusu shughuli za usafishaji na upimaji wa mahindi zinazofanywa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Rais samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Mapinduzi (CCM) amesema kuwa hatua hiyo inayolenga kuboresha maisha ya wakulima nchini ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Kwa mujibu wa maelekezo ya Rais, NFRA imeanzisha vituo vya ununuzi wa mahindi katika mikoa inayozalisha mazao haya kwa wingi, ikiwemo Ruvuma, Mbeya, na Njombe ikiwa na lengo la kuhakikisha wakulima wanapata soko la uhakika kwa mazao yao bila kulazimika kusafirisha umbali mrefu, hali inayowapunguzia gharama na adha za usafirishaji.

Aidha mpango huo unalenga kuwalinda wakulima dhidi ya wafanyabiashara walanguzi wasio waaminifu ambao wamekuwa wakinunua mazao yao kwa bei ya chini isiyolingana na thamani halisi ya mazao hayo huku NFRA ikiwa ni sehemu ya mkakati mpana wa serikali kuhakikisha kuwa mahindi yanayozalishwa nchini yanafikia soko la kimataifa.


          

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA