Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene leo amemtembelea na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete nyumbani kwake Kawe Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Simbachawene amefikisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameahidi kuendelea kuwa pamoja na Viongozi Wakuu Wastaafu wa Kitaifa kwa maendeleo ya taifa.
Mhe. Simbachawene amesema Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ina jukumu la kutunza Viongozi Wakuu Wastaafu Kitaifa na Wenza wao, hivyo yuko tayari kuendelea kutekeleza jukumu hilo alilopewa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ufanisi.
Hali kadhalika, Mhe. Dkt. Kikwete amemshukuru Mhe. Simbachawene kwa ujio huo na kupongeza utaratibu uliopo wa kuwatembelea Wiongozi Wakuu Wastaafu wa Kitaifa kwa kuwa unawapa faraja, unaonesha thamani na mchango wao kwa maendeleo ya taifa.
إرسال تعليق