SEKTA YA MICHEZO NGARA YAZIDI KUPEPERUSHA BENDERA BAADA YA MBUNGE WAO KUFANYA TUKIO HILI

NGARA - KAGERA.

Mbunge wa jimbo la Ngara Ndaisaba Ruhoro ameendelea kumwaga Fedha za udhamini kwenye mashindano ya Ligi Daraja la Nne kwa miaka mitatu mfululizo katika Wilaya ya Ngara.


Hayo yamejiri Septemba 17,2024 baada ya Kamati Tendaji ya Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ngara (NDFA) kumpa pongezi na kumshukuru Mbunge wa Jimbo hilo la Ngara kwa kuendelea kuwa Mdhamini Mkuu kwa miaka Mitatu mfululizo na kutoa fedha za Uendeshaji na zawadi mbalimbali za washindi wanaofanya vizuri katika Ligi Daraja la Nne Wilaya ya Ngara.


Ikumbukwe kuwa Mwaka huu 2024 kwa kwa mabingwa wa Mashindano Mbunge Ruhoro ametoa Ng'ombe mmoja, Tsh 500,000 na Kombe, Kwa mshindi wa pili ametoa Ng'ombe mmoja na Tsh 300,000/= wakati Mshindi wa Tatu ametoa Ng'ombe mmoja na Tsh 200,000/= sambamba na mfungaji bora wa mashindano akipewa kiasi Tasilimu cha Tsh 20,000/=, Mchezaji Bora Tsh 20,000/=, Kipa bora Tsh 20,000/= na Timu yenye nidhamu Tsh 40,000/=


"NDFA tunaendelea kumshukuru kwa Ufadhili wake wa fedha za kuendesha Mashindano, Zawadi Tasilimu na Ng'ombe. Mhe. Ndaisaba George Ruhoro umeleta chachu ya kuimarisha na kuleta ushindani wa timu zaidi ya 16 zinazoshiriki Ligi yetu kila mwaka, kuibua vipaji Chipukizi pamoja na maendeleo ya vilabu kujipima malengo yao, mafanikio na Changamoto" Kauli ya Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Wilaya ya Ngara (NDFA) FM. Malulu

"Tunashukuru sana naomba tuendelee kushirikiana katika Mpira wa miguu na kuwasogeza mbele vijana wetu walioonekana kufanya vizuri ikiwa ni pamoja  na kuzifadhili timu zilizoibuka mabingwa kwenda kucheza ligi ya Mkoa Novemba 2024." Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Wilaya ya Ngara (NDFA) FM. Malulu



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA