SERIKALI KUTOA VIBALI VYA MISIMU KWA WAHAMIAJI KATIKA NGAZI YA WILAYA HASA ZA MIPAKANI PAMOJA NA MKAKATI KABAMBE WA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI



Na, Mwandishi Wetu - Dodoma.

Serikali imeendelea na huduma ya utoaji wa vibali vya wahamiaji na maandalizi ya kupeleka huduma hiyo katika ngazi ya Wilaya kwa kuanzia Wilaya za Mipakani ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu sheria taratibu za vibali hivyo ili kupunguza changamoto wanazokabiliana nazo.

Hatua hii inakuja baada ya kukamilisha ufungaji wa mfumo kwaajili ya utoaji wa vibali hivyo katika ngazi ya Mikoa kwa mujibu wa majibu yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni kufuatia swali la Mbunge wa Jimbo la Ngara Mkoani Kagera Ndaisaba Ruhoro Leo Septemba 06, 2024 Bungeni Jijini Dodoma alilouliza kuwa "Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa Vibali vya Msimu katika Ofisi za Uhamiaji ngazi za Wilaya?." 

"Serikali kupitia Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 Rejeo la 2016, ilifanya marekebisho ya Kanuni za Uhamiaji za Mwaka 1997 kwa ajili ya kuzingatia haki za kundi la wageni hasa kutoka nchi jirani wanaoingia nchini kufanya vibarua hususan katika sekta ya kilimo na nyinginezo za msimu." Amesema Masauni

"Kupitia marekebisho hayo, Serikali ilianzisha aina maalumu ya kibali cha msimu yaani “Seasonal Migrant Pass” kupitia GN Na.518 ya mwaka 2018 ambacho hutolewa kwa wageni hao kwa kipindi cha kuanzia miezi mitatu hadi sita ili kuendana na msimu wa kilimo katika mwaka husika." 

Kutokana na Sababu kubwa ya wananchi wa Jimbo la Ngara kuwa wahanga wakubwa kwa kukabiliana na changamoto ya kutofahamu sheria, kanuni na taratibu za vibali vya misimu ikamuibua mbunge huyo kuuliza swali la nyongeza la kutaka kujua ni upi mkakati wa serikali kupeleka elimu kwa wananchi hao.

Waziri Masauni imebainisha kuwa Serikali imeandaa utaratribu Na Jeshi la uhamiaji Tanzania na Jeshi la Uhamiaji wa Nchi Jirani kutoa elimu kwani zina wajibu wa kuelimisha wananchi wao na kufafanua changamoto iliyopo kwa mfano.

"Miongoni mwa changamoto zinazotokana na utoaji wa vibali hivi ni wananchi kukosa elimu juu ya umuhimu wa kuwa na hati za kusafiria kutoka katika nchi zao, jitihada na mkakati umeshaandaliwa kati ya Chombo cha Nchi yetu na Nchi jirani wakati jitihada za kutoa elimu zikiendelea" Amesema Waziri Masauni



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA