Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini
katika Mwaka 2024/25 imepanga kufanya
usanifu wa kina kwa kilomita zote 9.87 za barabara ya Sadala - Uswaa na mara baada ya usanifu
kukamilika na gharama halisi za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa
ajili ya kuanza ujenzi huo kwa kiwango cha lami.
Majibu hayo yametolewa na Naibu waziri Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe.
Zainab A. Katimba Leo
Septemba 4,2024 Bungeni Jijini Dodoma, wakati
akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Mafuwe
alilouliza kuwa “Je, lini Serikali itatekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais ya
kujenga Barabara ya Sadala - Uswaa kwa kiwango cha lami?”
Naibu Waziri Katimba amesema katika mwaka 2023/24 barabara hiyo
ilifanyiwa matengenezo ya sehemu korofi
kwa gharama ya Shilingi milioni 26.8 na Mwaka 2024/25, Shilingi milioni 35 zimetengwa
kwa ajili ya matengenezo ya maeneo korofi.
Kufuatia majibu hayo ya Serikali yakamuibua Mbunge huyo
kuuliza maswali ya nyongeza kwa kutaka kujua ni lini utekelezaji huo utafanyika
kwani barabara hiyo ni ya ahadi ya muda mrefu Tangu Rais Mstaafu Hayati
Benjamini Mkapa na hata Rais wa Awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassani alipofanya
Ziara Mkoani humo alitoa ahadi ya kukamilisha barabara hiyo kwa kiwango cha
Lami.
Hata hivyo Serikali imesema kwa mwaka wa fedha 2024/25
imetenga kiasi cha shilingi Milioni thelathini na tano kwaajili ya matengenezo
katika sehemu korofi na mara baada ya usanifu kukumilika katika mwaka wa fedha
2025/26 itaingizwa katika mipango ya kujengwa katika kiwango cha lami.
إرسال تعليق