WANANCHI WAFUNGUKA MAKUBWA UJIO WA MATIKO FOUNDATION

 


Na Mwandishi Wetu - Mara.


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe. Esther Matiko amezindua Taasisi ya Matiko Foundation - MF itakayosaidia kutoa misaada ya kijamii kwa wakazi wa Wilaya ya Tarime na Tanzania kwa ujumla.


“Nikiwa na taasisi hii nitafanya vizuri zaidi katika kusaidia jamii ya Tarime na Tanzania kwa ujumla,” Esther alisema katika hafla ya uzinduzi wa taasisi yake Septemba 25, 2024.


Esther ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, pia aliupatia Umoja wa Wakuu wa Shule za Tarime msaada wa mashine ya Kuchapisha  mitihani yenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni 12.


Alisema suala la uhifadhi wa mazingira litapewa kipaumbele na taasisi hiyo, ambapo pia alitumia fursa hiyo kutoa msaada wa majiko ya gesi 60 kwa shule za msingi zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.


“Pia nimekuja na katoni 70 za ‘sanitary pads’ kwa ajili ya wanafunzi wa kike,” aliongeza Esther.


Pamoja na mambo mengine, inasadia kutetea haki za watoto ili waweze kufikia ndoto zao kielimu, kutangaza utalii na kuendeleza michezo Moani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi alimpongeza Matiko kwa kuanzisha taasisi hiyo, “Kwa namna pekee nimpongeze Mheshimiwa Mbunge  kwa kupata wazo la kuanzisha asasi hii muhimu katika jamii yetu. Hongera sana,” alisema Kanali Mtambi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.


"Katika zoezi ambalo limefanyika leo kwenye uzinduzi wa Matiko Foundation nipende kumpongeza Mbunge wetu Esther Matiko kwa namna ya kipekee ameendelea kutambua thamani na umuhimu wa elimu katika jamii kwa upande wa wanafunzi wa jinsia ya kike kwa kuzuia swala zima la ukeketaji katika jamii yetu na kuelemisha wazazi wetu.


Pia nimpongeze kwa kutambua thamini ya mtoto wa kike kwenye elimu lakini pia nimkumbushe kuwa kuna upungufu wa vitabu katika shule zetu hivyo niombe alione hili na kulipa kipaumbelee ,"Amesema Josephine  Nashoni Mwanafunzi Kutoka Shule ya Sekondari Nyamisangura






Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA