Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Bw: Silvest Arumasi akitoa hati ya shukrani kwa Bi. Twaiba Msechu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi la Ubungo
Na Mwandishi wetu Dar es salaam
Akiba Commercial Bank Plc imewashukuru wateja wake kuungana nao katika safari hii ya kutoa huduma bora zaidi za kibenki ambazo zinachangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania.
Shukrani hizo zimetolewa leo Octoba 9,2024 Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji waIBA benki ya Akiba Commercia Bw Silvest Arumasi katika Maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa wateja hafla iliyofanyika tawi la Ubungo la benki hiyo na kuhudhuriwa na Wateja wafanyakazi wa benki , na wawakilishi wa vyombo vya habari.
Mkurugenzi amesema wiki ya huduma kwa wateja wameifanya kwa namna ya kipekee kwa kutambua thamani ya wateja kwa kutoa tunzo kwani kufanya hivyo ni kuonesha ahadi ya benki ya kuendelea kutoa huduma bora.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Above and Beyond” ikimaanisha kwenda zaidi ya matarajio, kauli ambayo inakusudia kuhamasisha utoaji wa huduma bora zaidi kwa wateja.
“Niwashukuru wateja wetu kutuchagua kuwa washirika wenu wa kibiashara kwani bila nyinyi , tusingeweza kufikia mafanikio haya tunayojivunia leo hivyo wiki hii ni maalum kwa ajili yenu, tunathamini na kutambua mchango wenu ” amesema Arumasi
Hata hivyo Akiba Commercial benki imefanya maboresho yaliyofanyika katika huduma za kidijitali za benki, ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za ACB Mobile na Akiba Wakala kwa kuzingatia mahitaji ya wateja.
Akiba Commercial benki inafanya huduma mpya ya Internet Banking inayopatikana kwa wateja binafsi, makampuni makubwa, na taasisi mbalimbali, kama sehemu ya mkakati wa mabadiliko ya kidijitali wa benki hiyo kwa kauli mbiu “Twende Kidijitali.”“Kwa kuzingatia mabadiliko ya haraka ya kiteknolojia.
" Mwaka 2024 tumeamua kuupa jina la Mwaka wa Kidijitali,’ na tumejidhatiti kuwafikishia huduma za kibenki kwa njia ya kisasa zaidi kupitia mifumo yetu ya kidijitali,” aliongeza Bw. Arumasi.
Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja, Akiba Commercial Bank inafanya shughuli mbalimbali katika matawi yake yaliyopo Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Mbeya, na Dodoma ili kuwapa wateja fursa ya kuona na kushiriki katika maboresho yanayoendelea kufanywa.
Aidha Benki itaendelea kukusanya maoni na mapendekezo kutoka kwa wateja ili kuboresha bidhaa na huduma zake kwa ujumla.“Wiki hii siyo tu kwa ajili ya sherehe, bali ni ahadi yetu ya kuendelea kuboresha na kutoa huduma bora ambazo zitazidi matarajio yenu,” amesema Bw. Arumasi. “
إرسال تعليق