Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, ameratibu maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani yaliyofanyika tarehe 5 Oktoba 2024 katika Uwanja wa General Tyre, mkoani Arusha, ambapo walimu wapatao 4,954 kutoka shule za msingi na sekondari, za binafsi na serikali, walikabidhiwa zawadi ya majiko ya gesi kama sehemu ya juhudi za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Gambo amesema kuwa mpango huu ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kusukuma mbele ajenda ya nishati safi ya kupikia nchini.
Kuhusu zawadi za majiko ya gesi kwa walimu, Gambo alibainisha kuwa ilikuwa ni hatua muhimu ya kuthamini mchango wa walimu katika maendeleo ya taifa, huku pia wakitumika kama mabalozi wa matumizi ya nishati safi.
Katika kutambua zaidi mchango wa walimu, Gambo ametoa mashine nne za kurudufu (photocopy machine) kwa walimu jijini Arusha ambazo zitasaidia uchakataji wa kiwango kikubwa wa mitihani ya pamoja ya shule mbalimbali jijini humo.
إرسال تعليق