MRADI WA TUINUKE PAMOJA KUTOKOMEZA CHANGAMOTO ZA USAWA WA KIJINSIA DODOMA


Na, Mwandishi wetu - Dodoma.

Mradi wa Tuinuke pamoja unaotekelezwa Kwa ushirikiano na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) umekusudia kutatua changamoto za kijinsia katika maeneo mbalimbali nchini zilizopo katika jamii na kuwainua wanawake, kwa kuanza na Mkoa wa Dodoma.ambapo kupitia vikundi watapeleka rasilimali ili kusaidia kutatua changamoto hizo.

Hayo yamebainishwa leo 24 Oktoba, 2024 Jijini Dodoma Nestol Mhando, Meneja wa Mradi huo wakati wa semina husika ambapo amebainisha kuwa katika vikundi vilivyopo kwenye jamii watakuwa wanahakikisha wanavijengea uwezo ili kuwa na Taaluma stahiki kwenye utekelezaji wa miradi hiyo ambayo watakuwa wameibuni.

Aidha, eneo lingine kubwa katika Mradi huo ni kuviunganisha vikundi pamoja na mitandao inayohusiana na masuala ya usawa wa kijinsia ili kujadili Haki za wanawake, watoto na watu wote kwenye Jamii.

Naye Monica John, Afisa Habari kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania na mratibu wa Mradi huo ameeleza kuwa Mradi huo utafanyika katika Wilaya zote za Dodoma ndani ya kipindi cha miaka mitatu na lengo ni kuwezesha vikundi katika ngazi ya jamii kuweza kuwa na harakati za pamoja zitakazowezesha kuleta usawa wa kijinsia.

Upande wa Serikali umewakilishwa na Onolata Michael Rwegasira ambaye ni Afisa Maendeleo ya jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma yeye ametoa Wito kwa wananchi kuungana kwa pamoja bila kutegemea kuendelea kusaidiwa badala ya kujiinua wao kwa wao.

Mshiriki katika semina hiyo Michael Salali ameahidi kuwa wao kama wadau watahakikisha wanapeleka semina kwenye Jamii kuanzia ngazi za chini ili vikundi vya kijamii viweze kufanya uchechemuzi na kutengeneza usawa wa kijinsia.







Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA