MSAADA WA TAASISI YA NVeP NA BARRICK WAENDELEA KUNUFAISHA TAASISI ZA KIJAMII NCHINI

Wawakilishi wa vikundi vya kijamii vilivyopata msaada kutoka taasisi ya Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), wakiwa katika picha ya pamoja na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow (katikati) baada ya kukabidhiwa hundi (dummy cheque) katika mgodi wa Bulyanhulu karibuni.
Mkuu wa shule ya Sekondari Bulangwa Sane Machembe akionesha mfano wa hundi aliyokabidhiwa katika hafla hiyo.
Kaimu Meneja Mkuu Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Damian Brice­ Houseman,(kulia) akimkabidhi Mkuu wa shule ya Sekondari Bulangwa Sane Machembe mfano wa hundi ya dola 10,000 zilizotolewa na taasisi ya taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
Kaimu Meneja Mkuu Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Damian Brice­ Houseman,(kulia) akimkabidhi Mkuu wa shule ya Sekondari Bulangwa Sane Machembe mfano wa hundi ya dola 10,000 zilizotolewa na taasisi ya taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa shule ya Sekondari Bulangwa Sane Machembe (katikati) akibadilishana mawazo na Maofisa Waandamizi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu.


***
Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick, imetoa msaada wa dola za Kimarekani 10,000 kwa shule ya sekondari ya Bulangwa iliyopo mkoani Geita kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kukuza taaluma.

 Hivi karibuni vikundi vya kijamii vya Enterprise and Rural Development Community Initiative, Sudama, na Jamii yetu Development & Relief Agency kila moja pia kilipata msaada huo ambao ulikabidhiwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, alipokuwa kwenye ziara ya kikazi nchini.

Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake, watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.

Kila robo ya mwaka taasisi ya NVeP, imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii mbalimbali zenye uhitaji barani Afrika na kufikia sasa zaidi ya mashirika 25 yasiyo ya Kiserikali na taasisi za kijamii nchini yamepatiwa msaada huo na tayari umeleta mabadiliko chanya katika jamii hususani katika sekta ya elimu, afya kwa Wanawake na watoto na utunzaji wa Mazingira.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa shule ya sekondari ya Bulangwa, katika hafla fupi iliyofanyika katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Kaimu Meneja wa Mgodi huo, Damian Brice Houseman, aliipongeza shule hiyo kwa kufanikiwa kupata msaada huu wakati wa awamu hii na kusema kuwa taasisi ya NVeP, itaendelea kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi ambazo zinatoa huduma kwa jamii kwendana na malengo ya taasisi hiyo sambamba na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Akiongea baada ya kupokea hundi ya fedha za msaada huo, Mkuu wa shule ya sekondari ya Bulangwa, ameshukuru Barrick kwa msaada huo na kueleza kuwa utasaidia kuboresha miradi ya kuinua taaluma shuleni hapo na kupandisha ufaulu wa wanafunzi ili waweze kukabili changamoto mbalimbali kwa kutumia elimu bora wanayoipata.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA