Watu nane wamefariki dunia na wengine 36 wamejeruhiwa baada ya basi la abiria mali ya Kampuni ya Nyehunge kugongana na basi la Asante Rabi alfajiri ya saa 12 Oktoba 22,2024 katika eneo la Ukiriguru Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo chake ni mwendokasi.
Amesema ajali hiyo imetokea baada ya basi la Asante Rabi lenye namba za usajili T458 DYD lilokuwa likitokea Mwanza kuelekea Jijini Arusha kujaribu kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari na hivyo kuligonga basi la Nyehunge.
CHANZO NIPASHE.
إرسال تعليق