Kama ambavyo imekuwa ikifanya miaka ya nyuma, Kampuni ya Barrick nchini, mwaka huu tena inaungana na Serikali na wadau mbalimbali nchini katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kupitia migodi yake ya North Mara na Bulyanhulu.
Kampeni hizo zilizozinduliwa leo Novemba 25,2024 zitahusisha kutoa elimu dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia,ushauri wa kisheria na umuhimu wa utunzaji mazingira na matumizi ya nishati mbadala kwa wananchi wanaozunguka migodi yake.
Wafanyakazi wa Barrick wameshiriki uzinduzi wa maadhimisho hayo jijini Dar es salaam sambamba na kuunga mkono jitihada za kufanikisha maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka na kuhusisha wadau mbalimbali.
Wilayani Tarime maadhimisho hayo yamezinduliwa kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Nyamongo, yakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Flowin Gowele na yameandaliwa kwa ushirikiano mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Jeshi la Polisi na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, miongoni mwa wadau wengine.
Katika hotuba yake, Meja Gowele, amewaomba wanajamii wote kushiriki katika mapambano ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, ukiwemo ukeketaji wasichana na amewataka wazee wa mila na ngariba (wakeketaji) kuacha kuhamasisha ukeketaji kwani vyombo vya dola vimejipanga kukamata na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watakaobainika kukaidi katazo hilo la serikali.
Meja Gowele, ametumia nafasi hiyo kuushukuru na kuupongeza mgodi wa North Mara akisema Serikali inatambua na kuthamini mchango wake katika kutatua changamoto za wananchi.
“Mgodi wa North Mara umekuwa mstari wa mbele katika kuhudumia jamii, ninawaomba wananchi tuendelee kuuunga mkono kwa kazi kubwa unayofanya,” amesema.
Awali, Afisa Polisi Jamii Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jumanne Mkwama amewaomba wazee wa mila kuacha kujihusisha katika hukumu za kesi za ukatili wa kijinsia, badala yake washirikiane na vyombo vya dola kukomesha vitendo hivyo vya ukiukaji wa haki zabinadamu.
Katika kampeni hiyo ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, wadau mbalimbali watashirikiana kuendesha midahalo na mikutano ya kuelimisha jamii madhara ya ukatili wa kijinsia, miongoni mwa mada nyingine.
Mbali na Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Tarime na mgodi wa North Mara, wadau wengine walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo wakiongozwa na Jeshi la Polisi, ni wazee wa mila, ngariba, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, yakiwemo ATFGM Masanga, HGWT, VSO na timu ya wanasheria kutoka Bowmans.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Apolinary Lyambiko akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Apolinary Lyambiko akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Flowin Gowele akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Flowin Gowele akizungumza katika uzinduzi huo.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia jambo wakati wa uzinduzi huo.
Viongozi wa Serikali na mgodi wa North Mara katika pichaya pamoja na wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia wilayani Tarime.
Viongozi wa Serikali na mgodi wa North Mara katika picha ya pamoja na baadhi ya wazee wa mila waliohudhuria uzinduzi huo.
Viongozi wa Serikali na mgodi wa North Mara na baadhi ya ngariba (wakeketaji) waliohudhuria uzinduzi huo.
إرسال تعليق