Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mwanza, Gloria Mwaikambo akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeendesha semina kwa waandishi wa habari kutoka Kanda ya Ziwa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuelimisha umma kuhusu majukumu ya benki hiyo na masuala ya kifedha.
Semina hiyo ya siku mbili inafanyika katika Ukumbi wa BOT Tawi la Mwanza, na inahusisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera, Simiyu, Mara na Geita.
Akifungua semina hiyo leo Jumatano Novemba 14,2024 Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mwanza, Gloria Mwaikambo amesema lengo kuu la semina hiyo ni kukuza uelewa wa waandishi wa habari kuhusu majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania, ili kuweza kuandika habari na makala kwa usahihi na kuelewa vizuri masuala ya uchumi na fedha.
Pia inalenga kuwafahamisha waandishi wa habari kuhusu maendeleo mapya katika sekta ya fedha, ikiwa ni pamoja na sera na mikakati ya kisekta inayotekelezwa na Benki Kuu.
Malengo mengine ni kujenga mtandao wa waandishi wa habari za uchumi na fedha, kwa lengo la kukuza uandishi wa makala hizi na kufikia kiwango cha ubobezi pamoja na Kukuza uhusiano kati ya Benki Kuu na waandishi wa habari, ili kuongeza ufanisi katika kuelezea na kusambaza taarifa sahihi kwa umma.
"Hii ni semina ya kipekee, na tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana katika siku hii muhimu. Kwa zaidi ya miaka 12, Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikifanya semina za aina hii katika mikoa mbalimbali nchini, ikijumuisha Kanda za Mashariki, Kusini, Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kaskazini Nyanda za Juu, pamoja na Visiwani Zanzibar. Hata hivyo, leo hii ni mara ya kwanza semina hii kufanyika hapa Kanda ya Ziwa, na kwa hakika, ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati yetu. Tunatarajia kuwa semina hii itakuwa na manufaa makubwa kwetu sote",ameeleza Mwaikambo.
"Tangu Benki Kuu ilipoanza kutoa semina hizi, tumeshuhudia mabadiliko makubwa katika ubora wa kazi zinazofanywa na waandishi wa habari zinazohusu Benki Kuu na sekta ya fedha. Hii ni ishara nzuri kwamba tumeweza kufanikisha lengo letu la kuwajengea uwezo waandishi wetu wa habari. Benki Kuu imekuwa ikisikika kwa usahihi zaidi kupitia vyombo vya habari, na tumekuwa na ushirikiano mzuri na waandishi wa habari",ameongeza.
Amezitaja Mada zitakazotolewa na wataalamu wa BOT kwenye semina hiyo ya siku mbili kuwa ni pamoja na Muundo na Majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania, Maana ya Sera ya Fedha inayotumia Riba ya Benki Kuu, Umuhimu wa Benki Kuu kuwa na dhahabu kama sehemu ya akiba yake ya fedha za kigeni, Utekelezaji wa Sheria na Kanuni za Huduma Ndogo za Fedha, Uamuzi wa kuondoa noti za zamani katika mzunguko na Alama za usalama wa fedha na utunzaji wake.
"Mada hizi ni muhimu sana katika kuelewa zaidi kuhusu Benki Kuu, majukumu yake, na masuala mbalimbali yanayohusiana na sekta ya fedha na uchumi. Tunaamini kwamba kupitia semina hii, kila mmoja wenu atapata uelewa zaidi kuhusu Benki Kuu na michakato yake",ameeleza Mwaikambo.
Aidha ameweka wazi kuwa, Semina hizo zitaendelea kutolewa mara kwa mara, ili kuhakikisha waandishi wa habari wanapata uelewa mkubwa kuhusu majukumu ya Benki Kuu na sekta ya fedha.
"Tunaamini kuwa kupitia semina kama hizi, tutafanikiwa kuongeza ufanisi katika mawasiliano na kuhakikisha kwamba habari zinazohusu masuala ya fedha zinawafikia wananchi kwa usahihi.
"Benki Kuu inatambua na kuthamini mchango wenu mkubwa katika jamii. Waandishi wa habari nyinyi ni daraja muhimu kati ya Benki Kuu na umma wa Watanzania, kwa kupitia vyombo vya habari, makala, mahojiano, na vipindi mbalimbali. Tunaahidi kuendelea kushirikiana nanyi kwa faida yetu sote, na matarajio yetu ni kwamba semina hii itawafaidi sana ninyi, huku mkiendelea kutoa habari sahihi kwa jamii",ameongeza Mwaikambo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko, alisema kuwa semina hiyo inatoa fursa kwa waandishi kuwa na uelewa wa kina kuhusu masuala ya kifedha na sera za Benki Kuu, hivyo kusaidia kuongeza ufanisi katika ushirikiano kati ya vyombo vya habari na taasisi za kifedha.
Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mwanza, Gloria Mwaikambo akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa leo Jumatano Novemba 14,2024 katika ukumbi wa BOT Tawi la Mwanza - Picha na Kadama Malunde
Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mwanza, Gloria Mwaikambo akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa
Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mwanza, Gloria Mwaikambo akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa
Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mwanza, Gloria Mwaikambo akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa
Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano BOT Dodoma, Noves Moses akizungumza wakati wa semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa
Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano BOT Dodoma, Noves Moses akizungumza wakati wa semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza , Edwin Soko akizungumza wakati wa semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza , Edwin Soko akizungumza wakati wa semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa
Afisa Uhusiano Benki Kuu ya Tanzania Dodoma, Lwaga Mwambande akizungumza wakati wa semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa
Meneja Msaidizi wa Idara ya Uchumi BOT, Issa Pagari akitoa mada kuhusu Muundo na Majukumu ya BOT wakati wa semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa
إرسال تعليق