HAWA NDIO MAADUI WA CCM

Francis Haule

ASILI YA CCM

Historia ina bainisha kwamba  CCM kama chama cha siasa kilianzishwa  Rasmi mwaaka  05/02/1977.na hii ni kutokana na muunganiko wa kifalsafa na kimuundo wa Tanganyika African National Union(TANU) na Afro Shiraz Party (ASP)

TANU kikiongozwa na mwl.JULIUS K.NYERERE na kikiongoza upande wa Tanzania bara (Tanganyika) na ASP kikiongozwa na SHEIKH AMAN ABEID KARUME kikiongoza upande wa Tanzania visiwani(Zanzibar).


Misingi ya vyama hivi vya ukombozi  ilikuwa ni kuondoa unyonyaji na ukandamizwaji wa watu hasa wazalendo wa Afrika uliokuwa ukifanywa na watawala wa kikoloni na sera za kibepari(KIBEBERU) ambazo kwa kiasi kikubwa zilileta matabaka na uonevuu kwa watu wa zalendo.

Hivyo falsafa na madhumuni shabihiano ya vyama hivi vya ukombozi  ilichagiza kuundwa kwa chama kimoja cha siasa ambacho  ni Chama Cha Mapinduzi (CCM)

MALENGO YA CCM

Kama ilivyo kwa vyama vingine vya siasa dhumuni kuu la chama chochote cha siasa ni kushinda katika uchaguzi na kuunda dola na kuisimamia  dola  kwa ukamilifu.

CCM inalinda na kudumisha uhuru wanchi yetu Tanzania

Kuhimiza ujenzi wa ujamaa na kujitegemea(self reliant)

CCM ina simamia  utekelezwaji wa siasa,sera na ilani yake kwa wanchi na pamoja kueendeleza fikra za viongozi wa asisi wa vyama vya TANU na ASP


Nimuhimu kila mwana CCM afahamu kuwa CCM ndio chama pekee cha siasa hapa Tanzania chenye nguvu na uwezo wa kuunda dola na kuisimamia serilali ili kuleta maeendeleo kwa jamii.


MFUMO WA UONGOZI WA CCM

 CCM kama taasisi kubwa ya kisiasa ina mfumo wa uongozi unao fanana kuanzia  Tawi mpaka TAIFA.

Shina la wakareketwa-Tawi-kata-wilaya-mkoa –Taifa

Katika ngazi hizi zote kwa mujibu wa katiba ya CCM 1977  MFUMO wa uongozi una fanana na maamuzi ya vikao yana zingatiwa

Mwkit-katibu-katibu mwenezi-wajumbe wa kamati ya siasa- halimashauri kuu na mkutano mkuu.


IMANI NA MISINGI YA CCM

CCM inaamini katika

Usawa wa binadamu

Udugu 

Utu na heshima ya  mtu

Ujamaa na kujitegemea ndio njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa 


WAFAHAMU MAADUI WA  CCM  

Kwakuwa CCM ndio  chama kinacho ongoza nchi yetu tangu uhuru mpaka sasa  na kila jambo zuri na yale yenye changamoto ni matokeo ya usimamizi  wa sera na falsafa zake.


Baba wa Taifa  Mwalimu JULIUS K .NYERERE alibainisha kuwa Taifa letu lina maadui wa tatu ambao ni 

UJINGA----MARADHI ---NA  UMASKINI

Kwa kukuwa CCM kupitia sera zake  ndio inaongoza mapambano dhidi ya hawa maadui  kwa kusimamia utekelezaji wa sera,ilani na miongozo yake.

Tangu uhuru na kuasisiwa kwa Jamhuri ya muungano mwaka 1964 baada ya mapiduzi matukufu ya Zanzibar CCM imeendeleza jitihada za kuw ondoa na kuwatokomeza  hawa maadui.


ADUI UJINGA (IGNORANCE)

CCM Kama chama mathubuti cha siasa chenye malengo ya kuondoa adui ujinga kimeweza kusimamia serikali kutekeleza miradi ya utoaji elimu msingi mpa chuo kikuu kwa wana nchi  wote nchi nzima bara na visiwani

Kwenye hili tumeona shule za msingi na sekondari ziko kila kata , vijiji , maarufu kama shule za kata.

Pia vyuo vikuu vya serikali  vyenye ithibati ya kimataifa ikiwemo chuo kikuu cha DSM ,UDOM ,MZUMBE,SUA.Na vile vya binafsi ikiwemo 

ST.  AGUSTINO,MUM.

Pia sera ya elimu bila malipo kuanzia ngazi ya elimu msingi mpaka kidato cha sita na hata vyuo vikuu mikopo inayo tolewa na serikali  kwa kada zote 

Hii imepelekea ujinga kupungua kwa kiwango kikubwaa na kuzalisha wa talamu wengi  wa zalendo.

Shule zinazomilikiwa na CCM kupitia jumuiyaya wazazi nazozimetoa mchango mkubwa katika kupambana na adui ujinga mfano LUDEWA secondary school.

Kwa hili tuipongeze CCM kwa kusimamia vizuri sera na kuji pambanua kuwa ni chmaa ambacho kinaishi misingi yake kwa jamiii na kwa Taifa kwa ujumla


ADUI MARADHI.(DISEASE AND ILLNESS)

Ili jamii iweze kuzalisha na kushiriki kwenye shughuri za uzalishaji na maaendeleo ni muhimu ikawa na afya njema na kwa kutambua hili CCM kama chama tawala kime weka nguvu na jitihada kubwa kuhakikisha afya za watazanzania zina imarika.

Ujenzi wa Zahanati  na vituo vya Afya,hospitali  za wilaya na mikoa   katika  maeneo yote. Huu ni utekelezaji wa sera ,miongozo na ilani ya CCM katika kupambana na adui maradhi.

Pia kusomesha na kuendeleza taaluma ya Afya  kwa kudhaminiwa na serikali wakiwemo madaktari na wahudumu wa Afya kwa ujumla hii yote ni maeelekezo ya CCM ili kupambana na adui maradhi.

Programu ya madaktari bingwaa kwenda mikoani katika hospitali zote za wilaya ili maarufu kama madaktari wa SAMIA ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa. Huu ni uthibitisho kwamba CCM inafahamu maadui wake na inachukua hatua za kuwaondoa.

Bima ya afya kwa wote (NHIF)  Tumeshuhudia msukumo mkubwa wa serikali  ya CCM ikitoa msukumo na  hamasa na ikitunga sheriakupitia bunge kwa kila mtanzania kuwa na bima ya afya  kwa dhumuni la kuhakikisha kila mtanzania ana pata tiba.huu ni ushahidi tosha kuwa CCM ina pambana kuondoa adui maradhi .

ADUI UMASKINI  (POVERTY)

Ili kupunguza umaskini serikali ya CCM imekuwa na program ya TASAF ambayo imelenga kusaidia kaya maskini hii program imekuwa mkombozi wa  jamii na familia

 Uwezeshaji wa vijana ,akina mama ,na makundi malumu kupitia mapato ya ndani katika halimshauri za wilaya ,miji, na majiji.hii imesaida kwa kias kikubwaa kusaidia mitaji  kwa wajasiria mali wadogo na wa kati Kujikwamua kutoka hali ya umaskini na ukosefu wa mitaji ya biashara Kwa hili tuipongeze CCM kwa kuwajali wananchi.

Pia kumekuwa na mikakati mingi ikiwemo MKUKUTA na  MKURA BITA. hii yote ili lenga kupunguza ombwee la umaskini  kwenye jamii.


HITIMISHO.

CCM kama chama cha siasa kwakuwa madaraka yake yanatoka kwa wananchi  ndio maana CCM kupitia viongozi wa ngazi zote wana tumia   muda mwingi kuwa sikiliza wanchi na kutatua kero na changamoto zao

Na hii ndio turufu ya CCM kueendelea kujenga imani  kwawana  na uhalali wa kisisasI (Political legitimacy)  kwa wanchi kueendelea kukipa ridhaa ya kuongoza dola.

Ni ukweli usiopingika kwamba CCM ili indelee kueendelea kuaminika kwa wananchi ni lazima iendelee kuwa karibu na wananchi, kwa kuwasiliza changamoto zao na kuzi patia ufumbuzi  na pia  kuyasemea mazuri yote yanayofanywa na serikali.


Imeandikwa na

John Francis Haule

Mkuu wa soko kuu la ARUSHA

SIMU. 0756717987 au 0711993907

Email haule46@yahoo.com


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA