Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Joseph Modest Mkude akizungumza Novemba 26,2024 na waandishi wa habari
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Joseph Modest Mkude akizungumza Novemba 26,2024 na waandishi wa habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga na msimamizi wa uchaguzi wa wilaya hiyo Bw. Emmanuel Johnson akizungumza na waandishi wa habari Novemba 26,2024
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga na msimamizi wa uchaguzi wa wilaya hiyo Bw. Emmanuel Johnson akizungumza na waandishi wa habari Novemba 26,2024
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga na msimamizi wa uchaguzi wa wilaya hiyo Bw. Emmanuel Johnson akizungumza na waandishi wa habari Novemba 26,2024
Na Sumai Salum - Kishapu
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga imekamilisha kwa asilimia 100% zoezi la maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa huku usalama ukiimarishwa wakati wote wa upigaji kura na kutangaza matokeo.
Akizungumza Leo Novemba 26,2024 na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya Joseph Mkude amesema jukumu alilonalo ni kuhakikisha wilaya inakuwa na amani na utulivu hivyo vyombo vya ulinzi na usalama viko imara na makini kutekeleza majukumu yao ya kimsingi katika zoezi la upigaji kura na kukamilika salama bila kuwepo na hali ya hatari.
Mkude amesema katika vituo vyote vya upigaji kura wameimarisha ulinzi kutoka kwa jeshi la polisi na askari wa akiba huku akitoa wito kwa wananchi kuchagua viongozi watakaowatumikia na kukataa rushwa kwani rushwa itapelekea kupata viongozi wasioleta chachu ya maendeleo katika maeneo yao.
"Ndugu wananchi wa Wilaya yote ya Kishapu hali ya upigaji kura lengo letu lilikuwa ni kuandikisha watu 106,805 lakini uandikishaji tumeandikisha watu 169,768 sawa na 101% hivyo tuendelee kuliombea taifa letu la Tanzania uchaguzi ufanyike na kumalizikia salama", amesema Dc Mkude.
Mkude ameongeza kuwa hali ya uchaguzi kwa mwaka huu ni tofauti na miaka iliyopita hiyo ni kutokana na uwepo wa mamlaka ya mji mdogo wa Kishapu mara baada ya uchaguzi hivyo kutakuwa na uchaguzi wa vitongoji peke yake kwa Kata ya Kishapu na Mwataga huku kata zingine wakichagua viongozi wa vijiji na vitongoji.
"Tutakuwa na doria ya mara kwa mara kuhakikisha wananchi wanakuwa salama na uchaguzi unakuwa wa huru na haki kwa kila Chama na kwa wapiga kura hivyo watu wenye makundi maalum msiwazuie kitimiza wajibu wao wa kikatiba tunayotimu itakayowasiaidia kwani mazingira kwao ni rafiki msimamizi wa uchaguzi amejipanga vizuri" ,ameongeza Mkude.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Bw. Emmanuel Johnson amesema zoezi la upigaji kura limekamilika kwa asilimia 100 hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi.
"Jukumu langu ni Kusimamia maandalizi ya uchaguzi serikali za mitaa mwaka 2024 maandaizi yote yako tayari na maeneo ya kiutawala yatakayofanyiwa uchaguzi ikiwa ni pamoja na jumla ya vijiji 117 na vitongoji 614, vituo vya kupigia kura viko kwenye maeneo ya vitongoji lakini kwa kutambua uwepo wa vitongoji vikubwa zaidi tumeongeza vituo 47 ili kuwarahisishia wananchi wetu kufika maeneo ya kupigia kura kwa hiyo tunavituo jumla vya kupigia kura 660", amesema Mkurugenzi.
Johnson amesema vyama vilivyosimamisha wagombea katika nafasi za mwenyekiti wa kijiji CCM kimeweka wagombea 117 sawa na asilimia 100% ya vijiji vyote, CHADEMA wagombea vijiji 38 sawa na asilimia 32.5% pamoja na Act wazalendo wagombea 2 sawa na 1.7%.
"Katika ngazi ya vitongoji tuna vyama vinne vilivyosimamisha wagombea ikiwemo Chama Cha Mapinduzi CCM wagombea 614 sawa na 100%,Chama Cha Demokrasia ba Maendeleo CHADEMA 118 19.2%,Chama Cha ACT Wazalendo 6 sawa na 1% na Chama Cha Wananchi CUF wagombea 2 sawa na (0.3%) na tumejipanga kuhakikisha wapiga kura wanatekeleza wajibu wao wa kikatiba na kisheria bila kuwa na kikwazo chochote na wasimamizi watakaokuwa kwenye vituo wameseminishwa kwa makini zoezi ni fupi halichukui muda mrefu wananchi wajitokeze kwa wingi", ameongeza Johnson.
Akizungumzia matarajio baada ya Kishapu kuwa mji mdogo kama ilivyotangazwa mwaka 2014 amesema kutakuwa na mwamko wa maendeleo na uchumi wa wananchi utaongezeka kutokana kwa kuwepo kwa ajira huku wakilenga kuwa mji kamili hapo baadae.
Baadhi ya wananchi wa Wilaya hiyo Aisha Manfred na Joseph Dotto wamesema wamejipanga kikamilifu kutimiza haki yao kikatiba kwa kupiga kura na kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo bila kujari itakadi za vyama.
Mkazi wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Aisha Manfred akuzungumza kuhusu alivyojipanga kushiriki kikamilifu zoezi la upigaji kura uchaguzi serikali za mitaa Novemba 27,2024
Mkazi wa Mwigumbi Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Joseph Dotto akizungumza kuhusu alivyojipanga kushiriki kikamilifu zoezi la upigaji kura uchaguzi serikali za mitaa ifikapo Novemba 27,2024 kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo katika maeneo yao
إرسال تعليق