Na. Catherine Sungura - Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amepata tuzo ya utendaji bora na kuwa miongoni mwa Watendaji Wakuu 100, akitambuliwa ni kinara katika tuzo hizo kwa mwaka 2024, katika kategoria ya Mtendaji Mkuu wa mwaka (CEO/MD of the year).
Tuzo hiyo imetolea usiku wa tarehe 24 Novemba,2024 katika ukumbi wa 'The Super Dome' Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe. Sharrif Ali Sharrif.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo Mhandisi Seff amewashukuru waandaaji wa tuzo hizo, Ofisi ya Rais-TAMISEMI pia watumishi wote wa TARURA na wadau wengine kwa ushirikiano wao katika utendaji wa kazi ambapo imemuwezesha kupata tuzo hiyo.
Tuzo hiyo inayojulikana kama ‘Top 100 Executive List Awards’ huandaliwa na Kampuni ya Eastern star Consulting Group na hii ni mara ya nne kufanyika tangu kuanzishwa nchini.
إرسال تعليق