SERIKALI YAELEZA JITIHADA INAZOCHUKUA KUWEZESHA MATUMIZI YA GESI KWENYE MAGARI

 


-Kapinga ataja  msamaha wa kodi asilimia 25 kwa injini za magari yanayotumia gesi asilia iliyotolewa 2023/2024.

-Aeleza Serikali ilivyojidhatiti kupeleka umeme kwenye maeneo yote nchini.

Na Mwàndishi Wetu 

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema kupitia Bajeti Kuu Serikali ya mwaka 2023/24 Serikali ilitoa msamaha wa kodi ya ushuru wa forodha (customs duty) asilimia 25 kwa injini za magari yanayotumia gesi asilia yanapoingizwa nchini. 

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Novemba 06, 2024 bungeni jijini Dodoma  wakati akijibu swali la la Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Grace Tendega aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali kupunguza baadhi ya kodi kwenye magari yanayotumia mfumo wa gesi ili Watanzania wengi waweze kuyaagiza.

 "Tuaendelea na hatua mbalimbali za kuhamasisha sekta binafsi kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye viwanda vinavyo tengeneza vipuri vinavyotumika katika kufunga mfumo wa matumizi ya gesi asilia kwenye magari na mitambo hapa nchini", Amesema Mhe. Kapinga 

 Kuhusiana na usambazaji  wa umeme Vijijini, Vitongojini na kwenye mitaa Mhe. Kapinga  amesema Serikali kupitia Wizara ya Nishati imejidhatiti kuhakikisha maeneo yote nchini yanapata huduma ya umeme.

Aidha, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Ester Matiko aliyetaka kufahamu mkakati wa Serikali katika kubadili magari yanayotumia mfumo wa dizeli kwenda kwenye gesi, Mhe. Kapinga amesema  Serikali inaendelea kuwekeza kwenye vituo zaidi ili kuhakikisha pia na magari yanayotumia dizeli yanaanza kutumia mfumo wa gesi.

Ameongeza kuwa kutokana na utofauti uliopo kati ya magari yanayotumia petroli na dizeli ilikuwa ni rahisi kwa Serikali kuanza na magari ya petroli kabla ya yanayotumia dizeli.

Akijibu swali la Mbunge wa Kondoa Mjini, Mhe. Ally Juma aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itapeleka Mradi wa umeme wa Vijijini kwenye Mitaa ya Tampori, Kwamtwara, Chemichemi, Chandimo, Dumi, Hachwi na Guruma - Kondoa, Mhe. Kapinga amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea na kazi ya utekelezaji wa miradi ya kupeleka umeme katika maeneo ya vijijini na vitongojini na vijiji vyote vya Jimbo la Kondoa Mjini vimefikishiwa umeme.

Ameongeza kuwa.,  Mitaa ya Tampori na Chemichemi itapatiwa umeme kupitia mradi wa kupeleka umeme kwenye Vitongoji 15 kwa kila Jimbo.  

Mhe. Kapinga  amesisitiza Serikali kupitia TANESCO na REA inaendelea kuratibu kazi za kusambaza umeme katika mitaa ya Kwamtwara, Chandimo, Dumi, Hachwi na Guruma  kulingana na upatikanaji wa fedha.
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA