SERIKALI YAWEKA WAZI IDADI MAJERUHI NA VIFO AJALI YA GHOROFA LILILOPOROMOKA KARIAKOO LEO

 













Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amethibitisha kutokea kwa kifo cha mtu mmoja na wengine 28 kuokolewa wakiwa wamejeruhiwa katika ajali ya kuporomoka kwa ghorofa iliyotokea asubuhi ya leo, Novemba 16 Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye eneo la ajali, Waziri Mkuu amesema serikali kupitia kwa vikosi vya uokoaji itahakikisha shughuli hiyo inafanyika mpaka watu wote waliokuwepo kwenye jengo hilo wakati wa ajali wanathibitika iwapo wako hai au wamefariki.

Nacho kikosi cha zimamoto na uokoaji kimesema kuwa kinaendelea na juhudi za kuwaokoa watu walionaswa kwenye vifusi ikiwa ni pamoja na kuwapelekea hewa ya oksijeni kupitia mipira maalumu ili kuwasaidia kupata hewa safi wakisubiri uokozi.

Shughuli ya uokoaji inaendelea katika kifusi cha ghorofa hilo lililokuw akatika makutano ya mtaa wa Kongo na Mchikichi
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA