URAIA PACHA NI HATARI KWA USALAMA WA TAIFA LETU

   

John Francis Haule

****

 Wengi tuliofika elimu ya sekondari tumejifunza  kwa kiasi maana ya uraia na dhana ya uraia pacha( dual citizenship)  na katika nchi yetu Tanzania    uraia wa Tanzania unasimamiwa na sheria  ya mwaka 1995 sura no 357 na imerekebishwa mwaka 2002 na  inaenda sambamba na kanuni  uraia ya mwaka 1997.

Sheria imeainisha wazi aina za uraia Tanzania ni tatu

 (A)Uraia wa kuzaliwa( citizenship by birth)                                                       (  B  ) Uraia kwa  kurithi ( citizenship by   registration)          

 (  C)Uraia  wa  tajinisi (citizenship by Naturalization)


Kwa mujibu wa haki za binadamu  kila mtu yuko huru  kufanya maamuzi hasa yanayohusu maisha yake hata  kujiamulia wapi pakuishi.  Wengi tuna  fahamu maana ya  liberty  as freedom  of an individual to live as you wish. Kwa tafsiri fupi  ni hali ya uhuru wa mtu kuishi kwa namna anavyoona inafaa .Hivyo mtu kuzaliwa katika taifa flani hakukulazimu kuendelea kuwa raia wa nchi asilia kwa maisha yako yote.

Kupitia dhana hii ya uhuru  ndio ina jenga msingi wa kuwa na hili suala la uraia pacha. ama hata kuamua kwa hiari kuwa urai wa nchi yeyote ambayo unaona inafaa kuishi na kujenga familia. Mfano  wengi raia wa mataifa hususani ya Afrika wana penda kwenda marekani ama  nchi za  ughaibuni  na hatimaye wengi wanachukua uraia wa nchi hiyo ya Amerika mfano mwana blogger  maarufu hapa Tanzania anayefahamika kwa jina la MANGE KIMAMBI ambaye  amechukua  uraia wa Amerika na sasa ni Mmarekani akifurahia haki za Kimarekani ila asili yake ni uchagani hapa Tanzania

 Pia ifahamike wazi kuwa mtu kuamua kuwa raia wa nchi nyingine na kukana uraia wako wa nchi  asili sio USALITI  bali ni haki ya kiutashi na  kutumia uhuru wake. 

Sote tunafahamu kuwa hii Dunia ni moja na hii  mipaka ya kiutawala imewekwa ili kurahisisha  shughuli za utawala na himaya . mfano bara la Afrika liligawanywa mnamo 1885 baada ya mkutano wa Berlin ili kukidhi matakwa ya  ma BEBERU  walio kuwa wakigombania  mali na kukuza himaya zao hapa Afrika (SCRAMBLE AND PARTITION) Hata  Geography inaeeleza kuwa  dunia yote ili kuwa pande moja la ardhi ila liligawanyika kutokana na nguvu (kani ya mvutano) ya asili na kuzalisha mabara 7 ambayo ukiyaweka pamoja yana kuwa sawa (Gig saw fit evidence)

Vitabu vitakatifu vinabainisha  kuwa  MUNGU alimuumba ADAM  na akaona si vema Adam awe peke yake akatoa ubavu na kumuumba EVA .(ADAM NA HAWA) sasa kama  sote ni matokeo ya uzao wa Adam na Eva  kwa nini tusiwe huru kuwa na uraia wa nchi zaidi  ya moja   na kuwa na haki zote zinazotolewa na nchi hizo. Hivyo uraia   pacha ni haki ya asili ya kila binadamu japo inapaswa kuwa na utaratibu mzuri wa kuiweka.


NINI MAANA YA URAI PACHA? Kwa ufupi ni  hali ya mtu kuwa raia au mwananchi anayetambulika kisheria na nchi zaidi ya mbili na kuwa na haki zote za kisheria. Tofauti kati ya uraia pacha na diaspora.


DIASPORA  ni raia wanao ishi nje ya taifa la asili ila hawajakana  utaifa wao ,wanaweza wakawa masomoni, Ama wana fanya shughuli flani  hivyo diapora ni wazalendo wa kweli wana manufaa kwa taifa letu ikiwemo  kukuza na kueeneza Kiswahili mfano huko nchini China kuna diaspora wengi wana fundisha Kiswahili. Wanaimarisha diplomasia ya kiuchumi (economic diplomacy) kwa kuhamasisha watalii na technolojia. Pia wana tuma fedha kwa ndugu jamaa na marafiki ambapo nchi inapata kodi hivyo wanaongeza pato la taifa na kuongeza makusanyo ya kodi  hivyo serikali imeweka mfumo mzuri wa kuwa saidia diaspora kwa kuwapa hadhi maalumu.

HADHI MAALUMU: Kwakuwa  suala la uraia pacha limekuwa kizumngumkuti na bado halina muafaka hivyo serikali kwa kutambua umuhimu na mchango wa raia wenye asili ya Tanzania iliamua  kwa hiari kuwa raia wa mataifa mengine imekuja na mbadala wa kuwa na hadhi malum  ambapo wata kuwa na  haki flani  ,ikiwemo  kuwa na vitamblisho maalum na kufanya uwekezaji hasa ule wa kimkakati mfano kuanzisha viwanda na taasisi zinazoweza kusaidia jamii na nchi kwa ujumla.

Hadhi malumu itasaidia  kuongeza pato la taifa  kupitia ushuru wa kurudi nyumbani pia itahuisha hali ya kuleta maarifa  nyumbani (technological transfer).

Kiukweli nyumbani ni nyumbani hata kama mtu akiukana uraia wa nchi asilia inakuwa tu ili  kukidhi vigezo vya kupata uraia wa taifa husika dhumuini ni kuhakikisha maslahi ya mhusika yanafikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi husika lakini moyo na dhamira inabaki kuwa kwenye taifa  la asili,hivyo hadhi maalum kwa wale walio chukua uraia wa nchi nyingine ni kitu cha kupongezwa.  Ni sawa na mtu ambaye ameweka makazi yake mjini lakini kila siku anawasiliana na watu wa nyumbani  hiyo tunaita home umbirical ties. Hivyo hadhi maalumu ni  mkakati mzuri wa kuwatumia hawa walio na uraia wa nchi hizo kwa maslahi ya taifa letu.

KWANINI  URAIA PACHA NI HATARI KWA USALAMA WA TAIFA LETU


Kwa mujibu wa somo la uraia (civics) Taifa lina undwa na vitu vii nne(components of Nation)

Watu (population)

Eneo la kiutawala(territory)

Mamlaka kamili ya kujitawala(sovereignity)

Kutambuliwa kimataifa(international recognition)       

Hivyo watu ni kitu muhimu sana kwa taifa lolote na watu hawa lazma waweze kuwa watiifu kwa mamlaka  na  utawala wa Taifa husika yani  soverenity of the state sasa ni vigumu sana kwa mtu kujigawanya kuwa mtiifu kwa mamlaka mbili.


Sheria  ya  uraia  ya Tanzania  kifungu  namba  357   ya mwaka 1995 inasema “Wote waliokana uraia wa Tanzania  watapoteza haki ya kuendelea kuwa raia wa Tanzania”

 Kama mtu akiwa na akili timamu bila kushinikizwa na yeyote akaamua kuukana uraia wa Taifa lake ni mtu wa kumuangalia kwa jicho la pekee sana. na sheria imeweka wazi kabisa ukiukana uraia na kuwa  raia wa nchi nyingine utakuwa umepoteza haki zote za kuwa Tanzania.

Hii sheria iko sawa sana ikiwa na dhumuni la kulinda usalama wa nchi yetu na heshima ya  Taifa huru linalojitawala bila kuingiliwa na taifa jingine(as sovereign state)

Kwa mujibu wa Profesa KABUDI PALLAMAGAMBA   akiwa bungeni alisema kuwa utafiti alioufanya unaonyesha  51% ya nchi duniani hazijaruhusu uraia pacha.


HATARI ZA URAIA PACHA KWA TAIFA

Una punguza uzalendo kwa Taifa la asili. Uzalendo ni hari ama hurka ya mtu kulipenda taifa lake kujitolea kulilinda na kulitetea katika mazingira mazuri na magumu mfano wakati wa vita wazalendo hupigana ili kulinda Taifa kwa hapa Tanzania mwaka 1978 tukiwa vitani zidi ya Nduli Amini Dada. Wazalendo walijitoa kulinda na kulitetea Taifa sasa kukiwa na raia wana uraia wa nchi mbili au zaidi  kiuhalisia huwezi simama  na taifa  na kulilinda na kulitetea. Hata historia inaonyesha 1938 huko Ujerumani  wa jewish waliamriwa kuondoka na walipokwa haki zote ikiaminika kuwa ni wasaliti wa taifa la ugerumani wakati wa vita vya pili vya dunia.  Kwa msingi huo uraia pacha ni hatari sana kwa usalama wa nchi yetu. Watu tuwe wazalendo tulipende taifa letu tujitoe.

 2..Unaondoa dhana ya utiifu kwa mamlaka ya nchi (Obedience to states sovereignity au loyality)  ili mtu uwe mtiifu ni lazima uwe na mamlaka moja unayo itii  hata kwenye Biblia  imenenwa you  can’t save two masters at once yaani huwezi watumikia mabwana wawili kwa pamoja. Kwenye hili ni dhahiri shairi kwamba mtu mmoja hawezi tii mamlaka za mataifa mawili kwa pamoja. Mfano raia mmoja mchezaji au msakata kabumbu anatakiwa na team ya taifa lake kuchezea team ya taifa  kwa muda huo huo ana inaitajika na taifa jingine atajigawaje  ili kutimiza wajibu huo kwa mataifa mawili kwa pamoja at once? Jibu ni kizungumkuti sasa nadhani  uraia pacha unahatarisha  hata maslahi ya nchi hivyo sheria yetu iko vizuri na iendelee kusimamiwa kama ilivyotungwa.

3..Inaondoa hadhi ya utaifa ama utambulisho wa taifa  (  National hood or Natinal identity) ni muhimu kujivunia kuwa na hadhi  ya taifa moja   sasa mtuu akiwa na uraia wa zaidi ya mataifa mawili akiiitaji kuji tambulisha ataijitambulisha kama raia wa nchi gani? Hata historia ina onyesha miaka ya 1880 kipindi cha ukoloni Taifa la Ufaransa likiwa na sera yake ya Assimilation policy wote waliokidhi vigezo walipewa kuwa raia wa Ufaransa wakiacha kuwa raia wa mataifa yao. Hii ni kukuza utaifa.na hata utamaduni wa taifa la asili una  dhoofikaa kwa  mtu kuwa na uraia wa nchi Zaidi ya moja. Hivyo tuendelee kusimamia sheria yetu  inayolinda  utaifa wetu.

   4…Unahatarishaa siri za taifa na desturi ya taifa.     Katika kila taifa kuna mambo ya wazi  kwa maslai mapamna ya taifa  na kuna idara nyeti za nchi zinaitajika kuongozwa na wazalendo wa kweli. Sasa uraia pacha unaweza sukumwa nahii  dhana ya haki zabinadamu ikapelekea  watu wenye uraia wa nchi mbili kufanya kazi katika vitengo nyeti mfano IKULU. Sasa hiyo kiuhalisia lazima ina weza vujisha siri za taifa kwa mataifa mengine ambayo hayana nia njema na taifa letu. Kwa msingi huo nimuhimu kueendelea na  huu utaratibu wa kuto ruhusu urai pacha hapa Tanzania.Pia hata raia ambao hawana asili ya Tanzania nao we have to be kin  Kwa kuwa umbirical  ties bado inaweza toa msukumo kwa siri za Taifa.Kwa hili tutoe pongezi kwa Viongozi wetu wakati wa ujenzi wa IKULU CHAMWINO walitumia wazalendo pekee kujenga majengo hayo maalum ya Taifa. Hivyo tuendelee na huu msimamo na sheria hii ni nzuri na ni ya kizalendo.

5. Unaondoa umoja wa kitaifa (Natinal unity and solidarity) Taifa letu nitaifa la  kijamaa ambalo lili asisi hii falsafa 1967 katika azimio la Arusha ambalo linaamini kuwa bina damu wote nisawa na kila mmoja astahili  heshima na kuthaminiwa utu wake . Na hii itikadi inadumu kwakuwa rai wa Tanzania wote tuko katika huu mwamvuli wa umoja na mshikamano na hii ideilojia itadhoofika endapo tuta ruhusu watu kuwa na  uraia pacha ambao hawatakuwa na morali ya kuenzi tunu hii muhimu ya Taifa

6.. Inaondoa  utambulisho wa taifa ikiwemo lugha. Taifa letu lina utambulisho wa Kiswahili kuwa lugha ya taifa  na tuna jivunia na kuitambulisha dunia kuwa Tanzania ndio chimbuko la lugha hii adhimu ya  Kiswahili na ni tamaduni pia sasa tukiruhusu uraia wa        pacha hao kama wameweza kuukana  uraia je? Kuhusu lugha watajivunia kweli? Hapa ni kuzuia  huu uraia pacha kwa nguvu zote na jitihada zote

   7.Unakanganya  mfumo wa mashtaka kwa wale wenye         makosa ya jinai  (it compromises judicial extradition or persecution) ikitokea mtu mwenye uraia pacha akawa ametenda makosa ya kijinai na akakimbia taifa moja na kwenda taifa jingine atahukumiwaje? Ili kuepukana na hili ni muhimu kuendelea kuukataa uraia pacha.

HITIMISHO

Kwa kuhitimisha uraia pacha hauna maslahi na faida kwa nchi ya asili zaidi sana ni maslahi ya mhusika tu ili akidhi vigezo vya kufikia matamanio yake ama malengo yake na sio malengo ya Taifa.

Malengo ya nchi yetu ni kuona Taifa hili linaendelea kuwa moja na linadumisha  misingi na miiko ya kihistoria na kuenzi MUUNGANO WETU .


          MAKALA HII IMEANDIKWA NA

JOHN FRANCIS  HAULE

;MKUU WA SOKO KUU  LA ARUSHA. (MARKET MASTER)

0756717987 AU 0711993907

EMAIL.haulej4@yahoo.com or haulej46@gmail.com

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA