WORLD VISION TANZANIA YAKABIDHI BIDHAA ZA AFYA KUKABILIANA NA KIPINDUPINDU WILAYA YA KISHAPU

  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Tanzania Shukrani Dickson akikabidhi bidhaa za afya kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile (kushoto) ili kusaidia mapambano dhidi ya Kipindupindu Wilayani Kishapu 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la World Vision Tanzania limeendelea na juhudi za kusaidia kukabiliana na changamoto za kiafya nchini ambapo limekabidhi bidhaa za afya zenye thamani ya Shilingi 5,428,311.4 kwa serikali ya Mkoa wa Shinyanga ili kusaidia katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu, hasa katika Wilaya ya Kishapu.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo Jumanne Novemba 12,2024 na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Tanzania, Shukrani Dickson, kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Shukrani amesema World Vision Tanzania inaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kuboresha huduma za afya na kusaidia jamii katika kupambana na magonjwa ya mlipuko, kama kipindupindu.

Ametaja baadhi ya vifaa vilivyotolewa, ikiwa ni pamoja na vidonge vya kutakasa maji ya kunywa (Chlorine tablets), Oral Rehydration Salt (ORS), Drips za maji, sodium chloride injection, gloves za matibabu, Dettol, Dextrose, na vifaa vingine vya kinga na tiba.

Pia, ameeleza kuwa shirika hilo linajizatiti pia katika kuhakikisha upatikanaji wa matanki ya maji kwa ajili ya kutibu maji na ndoo za kunawia mikono, hasa shuleni.

Shukrani ameweka wazi kuwa World Vision Tanzania inaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kuhakikisha jamii inapata huduma bora za afya na kuboresha mazingira ili kupunguza magonjwa na milipuko.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, amekiri juhudi hizo na kusema kuwa World Vision Tanzania ni miongoni mwa wadau muhimu katika mkoa wa Shinyanga, akisema kuwa shirika hilo limekuwa msaada mkubwa katika maeneo ya lishe, usafi wa mazingira, na afya kwa ujumla.

Amesisitiza kuwa kwa sasa mkoa unakabiliana na msimu wa mvua, na kuna hatari kubwa ya milipuko ya magonjwa ya kuhara, kutapika, na kipindupindu.

Ameongeza kuwa Wilaya ya Kishapu inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama, ambapo wananchi wengi hutegemea visima na malambo ambayo yanaweza kuwa na maji yasiyokuwa salama, hasa wakati wa mvua na kutokana na hali hiyo inaweza kuongeza uwezekano wa magonjwa ya kuambukiza, ikiwa hatua stahiki hazitachukuliwa.

Hata hivyo, Dkt. Ndungile ameeleza kuwa kwa sasa hakuna wagonjwa wa kipindupindu katika mkoa wa Shinyanga na kwamba elimu na tahadhari kwa jamii inaendelea kutolewa ili kuzuia milipuko ya magonjwa.

Amehamasisha umuhimu wa kujenga vyoo bora, matumizi bora ya vyoo, kunawa mikono, kuchemsha maji, na kutumia vidonge vya kutakasa maji kama sehemu ya juhudi za kuzuia ugonjwa wa kipindupindu na magonjwa mengine.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Tanzania Shukrani Dickson akikabidhi bidhaa za afya kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile (kushoto) ili kusaidia mapambano dhidi ya Kipindupindu Wilayani Kishapu - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Tanzania Shukrani Dickson akikabidhi bidhaa za afya kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile (kushoto) ili kusaidia mapambano dhidi ya Kipindupindu Wilayani Kishapu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile (kushoto) akimshukuru Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Tanzania Shukrani Dickson kwa kuchangia bidhaa za afya kwa ili kusaidia mapambano dhidi ya Kipindupindu Wilayani Kishapu
Sehemu ya bidhaa za afya zilizotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kusaidia mapambano dhidi ya Kipindupindu Wilayani Kishapu
Sehemu ya bidhaa za afya zilizotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kusaidia mapambano dhidi ya Kipindupindu Wilayani Kishapu
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Tanzania Shukrani Dickson akizungumza wakati akikabidhi bidhaa za afya ili kusaidia mapambano dhidi ya Kipindupindu Wilayani Kishapu
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Tanzania Shukrani Dickson akizungumza wakati akikabidhi bidhaa za afya ili kusaidia mapambano dhidi ya Kipindupindu Wilayani Kishapu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likikabidhi bidhaa za afya ili kusaidia mapambano dhidi ya Kipindupindu Wilayani Kishapu

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA