DC SHEKIMWERI ATAHADHARISHA WAVAMIZI TASNIA YA HABARI

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kulinda heshima ya taaluma yao, akitahadharisha kuhusu ongezeko la watu wasiokuwa na ujuzi wa uandishi wa habari ambao wanatumia mitandao ya kijamii kueneza taarifa zisizo za kweli na za kuchafua jamii.

Akifungua mkutano mkuu wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) unaoambatana na Mkutano wa Uchaguzi leo Jumatano, Novemba 4, 2024 katika ukumbi wa UCSAF Jijini Dodoma, Shekimweri amesema kuwa hali hii inachangia kuharibu taswira ya waandishi wa habari wa kweli na kuathiri hadhi ya taaluma hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo uliotanguliwa na Semina kuhusu Habari Potofu, Shekimweri amesisitiza umuhimu wa weledi na maadili katika tasnia ya habari, ili kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinabaki kuwa chanzo cha taarifa za kuaminika na zinazolinda maslahi ya umma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN 

"Upo umuhimu mkubwa wa waandishi wa habari kuzingatia miongozo ya kitaaluma na maadili ya uandishi wa habari. Watu wasiokuwa na elimu ya uandishi wa habari wamevamia fani hii na wanachafua taswira ya waandishi wa habari wa kweli. Ni muhimu kuhakikisha kwamba taaluma hii inaheshimiwa na wale wanaofanya kazi hii wanazingatia weledi na maadili",amesema.

Mkuu huyo wa wilaya ameeleza kuwa mitandao ya kijamii, licha ya kutoa fursa ya kutangaza taarifa kwa haraka, inapaswa kutumika kwa ustadi na umakini mkubwa.

Ameongeza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kutumia mitandao hii kwa manufaa ya jamii na kwa njia inayolinda amani na usalama wa taifa.

"Tunapaswa kuwa wazalendo na nchi yetu,na tuitumie vizuri mitandao namna ya kuripoti taarifa, tusipotoshe umma, taarifa zikiandikwa ndivyo sivyo kunaweza kuleta machafuko katika nchi yetu. Tutumie mitandao ya kijamii kwa uangalifu na weledi, na tuwe na jukumu la kuhakikisha kuwa tunalinda amani ya nchi yetu kupitia taarifa tunazozitoa," amesema Shekimweri.

Aidha, Shekimweri amesisitiza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kuwa wazalendo na kuhakikisha kwamba maslahi ya taifa yanazingatiwa katika kila taarifa wanayochapisha.

Amewahimiza waandishi wa habari kuwa na jukumu la kutangaza ukweli, huku wakiwajibika kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, ameipongeza MISA-TAN kwa kusimamia Katiba yao pamoja na kufanya Mkutano Mkuu, na kueleza kwamba taasisi ambazo hazifanyi mikutano haziwezi kusimama imara.

Naye Mwenyekiti wa MISA-TAN Salome Kitomari ambaye amemaliza muda wake kwa mujibu wa Katiba ya MISA -TAN, akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi, amesema kwa sasa ulimwengu upo kwenye Teknolojia kubwa ya kimtandao pamoja na matumizi ya akiri mnemba na hivyo kusababisha kuwepo na habari nyingi za upotoshaji.
Salome Kitomari 

“Kwa sasa tupo kwenye dunia ya mitandao ambayo ina mambo mengi, pamoja na matumizi ya akiri mmemba na kumekuwa na habari nyingi za upotoshaji, ndiyo maana tunafanya mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wa habari,ili tuwe makini na matumizi ya mitandao na akiri Mnemba, na wasitoe maudhui ya upotoshaji,”amesema Salome.

Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Albert Richard, akiwasilisha mada kuhusu mradi wa ujenzi wa Minara 758, amesema mpaka sasa imeshawashwa Minara 306 ambayo itanufaisha wananchi milioni 8.5 kuimarisha mawasiliano katika maeneo ya vijijini.

Mkutano wa MISA TAN ni jukwaa muhimu kwa waandishi wa habari kujadili changamoto zinazokabiliana na sekta ya habari, na kutafuta mikakati bora ya kuboresha uandishi wa habari nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN  leo Jumatano, Novemba 4, 2024 katika ukumbi wa UCSAF Jijini Dodoma - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mwenyekiti wa MISA - TAN, Salome Kitomari akizungumza kwenye Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mwenyekiti wa MISA- TAN, Salome Kitomari akizungumza kwenye Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mwenyekiti wa MISA - TAN, Salome Kitomari akizungumza kwenye Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mkurugenzi wa MISA - TAN, Elizabeth Riziki akizungumza kwenye Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mkurugenzi wa MISA - TAN, Elizabeth Riziki akizungumza kwenye Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri na washiriki wa Mkutano wa MISA- TAN wakipiga picha ya pamoja
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri na washiriki wa Mkutano wa MISA -TAN wakipiga picha ya pamoja
Mkurugenzi wa uendeshaji kutoka mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) Mhandisi Albert Richard akiwasilisha mada kuhusu mradi wa ujenzi wa Minara 758

Mwenyekiti wa MISA - TAN, Salome Kitomari akiongoza Mkutano mkuu wa MISA-TAN 
Wanachama wakiwa kwenye Mkutano wa MISA- TAN
Wanachama wakiwa kwenye Mkutano wa MISA- TAN
Wanachama wakiwa kwenye Mkutano wa MISA- TAN
Wanachama wakiwa kwenye Mkutano wa MISA- TAN
Wanachama wakiwa kwenye Mkutano wa MISA- TAN
Mwenyekiti wa MISA - TAN, Salome Kitomari akimpokea Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri (kushoto)

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA